Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Singida Black Stars ataja mbinu za ushindi

KIMOTO Pict

Muktasari:

  • Katika mechi sita za hatua ya makundi msimu wa 2025/26, Singida ilipata ushindi mmoja, sare mbili na kupoteza mechi tatu, ikifunga mabao matatu na kuruhusu sita. Ushindi wake pekee ulikuwa wa bao 1-0 dhidi ya AS Otoho ya Congo.

SINGIDA Black Stars imeanza kampeni  ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Tusker FC ya Kenya, huku kocha wake akiahidi mambo makubwa.

Katika mechi sita za hatua ya makundi msimu wa 2025/26, Singida ilipata ushindi mmoja, sare mbili na kupoteza mechi tatu, ikifunga mabao matatu na kuruhusu sita. Ushindi wake pekee ulikuwa wa bao 1-0 dhidi ya AS Otoho ya Congo.

Msimu huu, timu hiyo imeanza kwa kasi tofauti katika hatua za awali, ikifunga mabao 10 dhidi ya El-Ghazal ya Sudan Kusini na kisha kupata ushindi muhimu wa ugenini dhidi ya Tusker, Oktoba 18, 2026.

KIMO 02

Akizungumza na Mwanaspoti Kocha Papy Kimoto amesema ushindi huo haukupatikana kwa bahati, bali ulitokana na mbinu alizotumia kubadilisha mwenendo wa mchezo baada ya kuona kikosi chake hakikucheza vizuri kipindi cha kwanza.

“Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri kwetu, lakini tulifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwaingiza wachezaji ambao tunaamini wana uwezo wa kutengeneza matokeo. Tulihitaji kubadilisha hali ya mchezo na kutafuta bao,” amesema Kimoto.

Mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda dakika ya 52, wakati Jeancy Mboma alipofunga bao pekee lililoipa Singida ushindi huo muhimu ugenini. Bao hilo limeiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kuwania tiketi ya hatua ya makundi.

KIMO 03

Kimoto amesema pamoja na kupata ushindi huo, kikosi chake hakipaswi kujisahau kwa sababu bado kuna kazi ya kukamilisha nyumbani, huku akisisitiza Tusker ni timu yenye uwezo na inaweza kubadilisha matokeo katika mchezo unaofuata.

“Bado mechi haijaisha. Tusker ni timu nzuri na tunatakiwa kuwa makini sana. Ushindi huu ni muhimu kwetu, lakini hatupaswi kuingia kwenye mchezo wa marudiano tukiamini kwamba tayari tumefuzu. Tunahitaji kuendelea kujiandaa vizuri na kutekeleza mipango yetu.”

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Jumapili, tarehe 25 Oktoba 2026 kuanzia saa 1:00 usiku, huku Singida Black Stars ikiwa nyumbani ikihitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili mfululizo.