Prime
Kocha Simba aichorea ramani Yanga CAF
ALIYEKUWA kocha wa Simba, Dimitar Pantev, ameitazama Yanga ilivyocheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United na kusema timu hiyo inapaswa kufanyia kazi mambo mawili kabla ya mchezo wa marudiano.
Pantev ambaye alikuwa nchini Botswana wakati Yanga ikicheza mchezo huo, amesema kikosi hicho cha Manqoba Mngqithi kilionyesha baadhi ya upungufu ambao unapaswa kurekebishwa mapema kabla ya kukutana tena na Gaborone United wikiendi ijayo.
Katika mchezo huo wa kwanza uliopigwa Botswana juzi Jumamosi, Yanga ililazimisha sare ya bao 1-1, matokeo ambayo yanaifanya timu hiyo kuwa na kazi ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mchezo wa marudiano ili kufuzu raundi ya pili.
Kwa mujibu wa Pantev, moja ya maeneo ambayo Yanga inahitaji kuyafanyia kazi ni namna ya kutengeneza nafasi za kufunga, akieleza kuwa timu hiyo haikuwa na ubora wa kutosha katika eneo hilo.
“Yanga ilipata wakati mgumu katika kutengeneza nafasi. Ukiwa unacheza mashindano ya aina hii, lazima uwe na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi na kuzitumia pale zinapopatikana,” amesema Pantev.
Kocha huyo amesema tatizo hilo si la wachezaji pekee, bali ni eneo ambalo benchi la ufundi chini ya Mngqithi linapaswa kulifanyia kazi ili kuhakikisha timu inakuwa na ubunifu zaidi inapofika katika eneo la mwisho la uwanja.
Pantev anaamini kuwa Yanga ikiwa itaboresha namna inavyofikisha mpira katika eneo la hatari, inaweza kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kupata matokeo inayoyahitaji katika mchezo wa marudiano.
“Unapocheza dhidi ya timu ambayo imejipanga vizuri, huwezi kutegemea nafasi chache. Lazima utengeneze nafasi zako mwenyewe na uwafanye wapinzani waanze kucheza kwa presha,” amesema.
Mbali na suala la utengenezaji wa nafasi, Pantev ametaja jambo lingine ambalo Yanga inapaswa kuwa makini nalo katika mchezo wa marudiano, akisema ni namna ya kujilinda wakati inapopoteza mpira.
Kocha huyo amesema Gaborone United ina uwezo wa kufanya mashambulizi ya kustukiza na kwamba Yanga inapaswa kuwa na umakini mkubwa inapokuwa inasonga mbele ili isiachie nafasi kwa wapinzani kutumia kasi yao.
“Gaborone ni timu ambayo inaweza kukuadhibu kwa mashambulizi ya kustukiza. Yanga inapokuwa inashambulia, lazima iwe na mpangilio mzuri wa kujilinda kwa sababu kupoteza mpira sehemu mbaya kunaweza kuwa hatari,” amesema.
Kocha huyo ambaye siku chache zilizopita alikuwa nchini Tanzania kwa ajili ya kujiendeleza kitaaluma katika ukocha.