Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Simba afurahia ushindi

Muktasari:

  • Mchezo kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mchezo kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere na Benard Morrison katika vipindi vyote viwili huku bao la Dodoma Jiji lilifungwa na  Cleophas Mkandala.

Baada ya mchezo, Kocha wa Simba Didier Gomes alisema muhimu kwa timu yake ilikua ni kupata alama tatu tu bila kujali timu yake ilivyocheza.

"Nimefurahia ushindi huu ambao ni muhimu kwetu kuhakikisha tunasogea juu ya msimamo, japo mchezo ulikuwa mgumu kulingana na ubora wa wapinzani wetu" alisema Gomes.

Gomes pia alisema ushindi huo umempa nguvu zaidi ya kufanya vizuri mechi inayofuata dhidi ya Azam kutokana na kuwa mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu.

Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata alisema vijana wake walicheza kama alivyowaelekeza licha ya kufungwa.

"Wachezaji wangu wamecheza vizuri licha ya kufungwa licha ya kuwa na muda mfupi wa kujiandaa na mchezo huu" alisema Makata.