Kocha Rhino Rangers afichua jambo
Muktasari:
- Rhino ni mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2025-2026, baada ya kuifunga Bandari Tanzania iliyopanda kwa kuongoza kundi A na pointi 32 kwa penalti 4-2, kufuatia sare mabao 2-2, mechi iliyopigwa Juni 17, 2026.
KOCHA Mkuu wa Rhino Rangers ya mjini, Tabora, Salvatory Edward, amesema hadi sasa ni mapema kufanyia tathimini ya kikosi hicho, japo, kuna matumaini makubwa kabla ya kumaliza raundi ya kwanza, yanayowapa motisha ya kuendelea kupambana zaidi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Salvatory aliyewahi kuifundisha Yanga, KenGold FC, Biashara United, Pamba Jiji FC na timu ya taifa ya Tanzania, amesema raundi ya kwanza itakapomalizika, ndipo atakuwa na wakati mzuri wa kufanya tathimini vizuri.
“Ushindani uliopo kwa sasa siwezi kusema tumefanikiwa au bado kwa sababu Ligi haijafikia tamati, baada ya kucheza mechi 15, hapo ndipo nitakuwa na wakati mzuri wa kueleza tathimini yangu, hivyo, acha tuendelee kupambana,” amesema Salvatory.
Kabla ya mechi ya jana Jumapili dhidi ya Bandari Tanzania, timu hiyo imeshinda nne, sare tatu na kupoteza miwili kati ya tisa iliyocheza, ikiwa nafasi ya sita na pointi 15, huku wakifunga mabao saba na kuruhusu pia manne.
Rhino ni mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2025-2026, baada ya kuifunga Bandari Tanzania iliyopanda kwa kuongoza kundi A na pointi 32 kwa penalti 4-2, kufuatia sare mabao 2-2, mechi iliyopigwa Juni 17, 2026.