Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha KMKM alia na wachezaji

KMKM Pict

Muktasari:

  • KMKM jana Jumamosi ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ilikubali kichapo hicho katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ina kazi ya kufanya Septemba 12, 2026 katika marudiano huko Libya.

KOCHA Mkuu wa KMKM, Ali Vuai Sheni, amesema kichapo cha mabao 3-0 walichokipokea kutoka kwa Al Ahli Tripoli katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, ni makosa ya wachezaji.


KMKM jana Jumamosi ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ilikubali kichapo hicho katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ina kazi ya kufanya Septemba 12, 2026 katika marudiano huko Libya.

Mabao hayo yote yalifungwa kipindi cha kwanza ndani ya dakika saba wafungaji wakiwa ni Mahdou El Houni (dk 20), Fiston Mayele (dk 22) na Hocine Dehiri (dk 27).

Akizungumzia matokeo hayo, Vuai amesema kwa namna wapinzani wao walivyokuwa, kikosi chake hakikuwa na sababu ya kupoteza mechi hiyo, lakini kilichotokea ni wachezaji kufanya makosa.

“Hatukuwa na sababu ya kufungwa mabao yote yale, ilikuwa ni makosa ya wachezaji wenyewe ikiwemo udhaifu wa kipa,”.

Mbali na makosa yaliyojitokeza, kocha huyo amebainisha kwamba wachezaji waliopoteza mawasiliano ndani ya uwanja, huku pia hofu waliyokuwa nayo hasa kipindi cha kwanza pia imechangia matokeo hayo.

Alibainisha kwamba, baada ya kugundua hilo, kipindi cha pili walibadilika na kucheza vizuri, licha ya kutopindua matokeo huku akiahidi watajirekebisha kwenye uwanja wa mazoezi ili mechi ya marudiano wakiwa ugenini wafanye vizuri.

Naye, Kocha wa Al Ahli Tripoli, Hossam El Badry, amesema kwa usajili walioufanya msimu huu akiwemo Fiston Mayele na John Ebuka, wanalenga kushinda Kombe la Shirikisho Afrika.

Amesema, hiyo ni mechi yao ya kwanza kwa msimu huu, bado timu haijawa vizuri hivyo inahitaji muda wa kutosha kuunganisha kikosi kwa sababu wachezaji wengi ni wapya.

Timu hizo zitarudiana Jumamosi Septemba 12, 2026 nchini Libya.