Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha: Huyu Guede anafunga kama Mayele

Muktasari:

  • Yanga iliyoingiza straika huyo katika dirisha dogo sambamba na viungo washambuliaji, Augustine Okrah na Shekhan Ibrahim na mchezaji huyo mrefu wa mita 1.82 akiwa na umri wa miaka 29 anarajiwa kujiunga na timu hiyo wiki ijayo na kocha aliyewahi kumfundisha amemchambua kuwa jamaa anajua sana.

SIKU chache zimepita tangu Yanga kumsajili mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Joseph Guede, kocha wa ASEC Mimosas, Julien Chevailer amewatoa hofu wanayanga kwa kuwaambia wajiandae kufurahi kwani jamaa anajua kufunga kama Fiston Mayele.

Yanga iliyoingiza straika huyo katika dirisha dogo sambamba na viungo washambuliaji, Augustine Okrah na Shekhan Ibrahim na mchezaji huyo mrefu wa mita 1.82 akiwa na umri wa miaka 29 anarajiwa kujiunga na timu hiyo wiki ijayo na kocha aliyewahi kumfundisha amemchambua kuwa jamaa anajua sana.

Guede amewahi kucheza timu mbalimbali ikiwamo FAR Rabat ya Morocco inayonolewa kwa sasa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi na Tuzlapor ya Uturuki ambayo aliachana nayo miezi minne iliyopita.

Mshambuliaji huyo anayetumia zaidi mguu wa kulia amesajiliwa ili kuchukua nafasi ya Hafiz Konkoni aliyeshindwa kuziba pengo la Fiston Mayele aliyepo Pyramids ya Misri aliyeondoka akiwa kama Mfungaji Bora wa Ligi Kuu akifunga mabao 17 sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba, na kufunga pia saba katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita akiwa kinara wa michuano hiyo ambayo Yanga ilifika fainali.

Yanga iliamua kumsajili mshambuliaji huyo ili kuoiongezea nguvu safu ya timu hiyo iliyobebwa kwa sasa na viungo Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Stephane Azizi Ki anaeongoza kwa idadi ya mabao 10 na sasa anaenda kuungana na washambuliaji kama Kennedy Musonda na Clement Mzize.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Ivory Coast, Kocha Julien alisema anamjua vizuri mshambuliaji huyo tangu yuko FAR Rabat na ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mzuri wa kufunga.

Aidha alisema endapo mshambuliaji, Sankara Karamoko aliyekuwa akiwindwa na Yanga, angeondoka basi Guede ndiye angekuwa mbadala wake, kwani ana kipaji kikubwa akifanikiwa kurudisha kujiamini kwake basi atafanikiwa ndani ya Yanga na kuibeba kama ilivyokuwa msimu ulioopita ikiwa na Mayele.

"Nina imani kubwa kuwa atakwenda kuwa mshambuliaji mzuri na mwenye msaada katika kikosi cha Yanga kwani wanahitaji mtu wa aina yake, pia uwepo wa viungo wazuri utamsaidia zaidi kutengeneza nafasi za kufunga," alisema Julien na kuongeza;

"Kama mshambuliaji wetu (Sankara) Karamoko angeondoka basi nilikuwa nafikiria kumchukua, kwani naamini uwezo alionao, ifahamikie kuwa mchezaji yeyote hawi bora pekee yake inategemea na anacheza na nani kwani umoja wao ndio unaleta ushindi."