Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Ceasssia aanza tambo

CEACEA Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo ya mkoani Iringa ambayo ni msimu wake wa tano mfululizo ikicheza ligi hiyo kwa mafanikio, ilianza kwa kipigo cha 2-0 dhidi ya Alliance Girls na juzi ikiwa katika kiwango bora ikamalizia hasira kwa wapinzani hao.

CEASSIA Queens imeanza kujipata kufuatia ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Bunda Queens katika Ligi Kuu ya Wanawake, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Shaban Zanzibar akiwafungia kazi straika wake.

Timu hiyo ya mkoani Iringa ambayo ni msimu wake wa tano mfululizo ikicheza ligi hiyo kwa mafanikio, ilianza kwa kipigo cha 2-0 dhidi ya Alliance Girls na juzi ikiwa katika kiwango bora ikamalizia hasira kwa wapinzani hao.

Kwa sasa wawakilishi hao pekee Nyanda za Juu Kusini, inatarajia kurejea kibaruani tena Novemba 11 kuwakabili Tausi FC ambao hawajaonja ushindi wowote ikipoteza mechi mbili mfululizo.

Zanzibar amesema baada ya kupoteza mchezo wa ufunguzi walikaa na kujitathimini akifanyia kazi makosa ya straika wake ambao walionesha udhaifu kutumia nafasi na kufanikisha mpango huo uliozaa matokeo mazuri.

Amesema wakati akiendelea kuiongezea makali straika wake, anaendelea kujiuliza tatizo kwenye eneo la beki kuruhusu mabao mechi mbili mfululizo, kuhakikisha michezo inayofuata hawafanyi makosa.

“Lazima niangalie pia sehemu ya beki kwakuwa tumeruhusu mabao kila mchezo, straika wamebadilika ila hawajaonesha makali ninayotaka, kazi si nyepesi na lazima kuongeza nguvu ili mechi zinazofuata tuwe bora” amesema Zanzibar.

Amesema kuwa kwa sasa wanajiandaa na mchezo ujao ugenini dhidi ya Tausi jijini Mwanza, akieleza kuwa mabadiliko yaliyoonekana kikosini, matarajio yake ni kuondoka na pointi tatu kujiweka pazuri.