Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMKM yajipanga kuongeza nguvu ZPL

EPL Pict

Muktasari:

  • KMKM imefungwa mabao nane na kufungwa saba ikikusanya pointi 10 sawa na ilizonazo Raskazone iliyopo nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi hiyo. Timu hiyo itavaana na Uhamiaji Oktoba 29, 2026 kwenye uwanja wa Mao B uliopo Unguja.

KOCHA Msaidizi wa KMKM, Ibrahim Khamis Khatib amesema timu hiyo inajitahidi kutengeneza mashambulizi kwa wapinzani wake lakini inakuwa ngumu kumalizia.

Ibrahim amesema, timu hiyo ina uwezo wa kumaliza mchezo dakika 20 za kwanza lakini wachezaji wanashindwa kufanya hivyo baada ya kupoteza nafasi nyingi.

Alieleza kuwa, Anaamini bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika michezo ijayo na kuingia katika nafasi ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

“Nafasi ya kuwa mabingwa wa ligi bado tunayo kwa sababu tumetofautiana pointi kidogo, hivyo tunaendelea kujiimarisha kwa mechi zijazo,” amesema.

KMKM kwasasa ipo nafasi ya nane ya msimamo wa ligi hiyo ikifanikiwa kushinda mechi tatu kati ya nane ilizocheza, ikitoa sare moja na kupoteza michezo mitatu.

KMKM imefungwa mabao nane na kufungwa saba ikikusanya pointi 10 sawa na ilizonazo Raskazone iliyopo nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi hiyo. Timu hiyo itavaana na Uhamiaji Oktoba 29, 2026 kwenye uwanja wa Mao B uliopo Unguja.