Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klabu ligi kuu zaonywa kimataifa

Muktasari:

  • Tanzia imepata nafasi ya kushirikisha timu 4 katika michezo ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho Afrika (CAF) kutokana na Tanzania kukusanya alama nyingi zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Mpira wa Miguu  Afrika.

BAADA ya Tanzania kupata nafasi nne za ushiriki wa klabu katika michuano ya Afrika mwakani (CAF), mbili Ligi ya Mabingwa na mbili Kombe la Shirikisho, makocha wa klabu hizo wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na Tanzania kupata nafasi hizo.


Wakitoa maoni yao kwa wakati tofauti makocha wa klabu za Ligi kuu wamepongeza kwa hatua hiyo ila wakitoa nasaha kwa klabu ambazo zitapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

Kocha wa Kagera Sugar, Francis Baraza alisema kuwa ni hatua nzuri kwa ligi yetu kwani inazidi kuonyesha  ni kiasi gani inazidi kupiga hatua. alisema kuwa licha ya kupata nafasi hiyo ila sio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo bali tumekuwa tukipata nafasi hiyo mara kwa mara.

Alisema kuwa ni jambo la kufurahisha ila kwa sasa inabidi klabu zitakazoshiriki zihakikishe zinajipange vyema ili tuendelee kupata pointi nyingi ili tuendelee kusalia na timu nne.

"Sio mara ya kwanza kushirikisha timu nne katika michuano hii, ingawa ninachoweza kusema klabu zitakazopata nafasi ya kushiriki zihakikishe zinakuwa na maandalizi mazuri ili kuendelea kusalia katika nafasi ya timu nne kila msimu," alisema Baraza.

Naye kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata alisema kuwa anaipongeza klabu ya Simba kwani kwa jitihada zake katika michuano ya Kimatataifa imeifanya nchi kushirikisha tena timu nne, Makata alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikituongezea alama kutokana na ubora mkubwa ambao imekuwa ikiuonyesha.

Anasema kuwa ukiingalia Simba unaona kabisa ni timu ambayo imeandaliwa katika michuano hiyo, alisema angalia kwenye maboresho ya kikosi kwani kila msimu wanaingiza maingizo mapya kutokana na mapungufu wanayoyabaini.

"Klabu zinapaswa kuiga mfano kwa Simba kuelekea michuano hiyo kwa kuhakikisha zinajipanga vyema kuanzia kwenye usajili wa wachezaji wenye ubora ili kuendelea kudumu katika nafasi hizi nne kwa misimu ijayo," alisema

Aidha kocha wa Mtibwa Sugar, Badru Mohamed alisema kuwa timu ambazo zitapata nafasi ya kushiriki katika michuano hiyo zihakikishe zinajipanga vyema kwa kuandaa michezo ya kimataifa ya kirafiki ili kupata fursa ya kujipima vizuri kabla ya kucheza michuano hiyo.

Akitolea mfano klabu ya Simba ilipoandaa michuano ya (Simba Super Cup) kwa kushirikisha timu za nje ya nchi kwaajili ya kujipima kabla ya kuanza kwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

"Angalia timu kama Simba iliandaa mashindano yao kucheza na timu za nje, sio kwa lengo la kujifurahisha tu bali liikuwa kwa lengo la kujipa uzoefu na timu mbalimbali na kuangalia madhaifu ya kikosi chao ili wayarekebishe kabla ya kuanza kwa michuano hiyo mikubwa barani Afrika," alisema Badru

Pia kocha huyo alisema kuwa klabu ambazo zitapata nafasi ya kushiriki zifanye maboresho mazuri ya kikosi chao kwa mahitaji ya nafasi ambazo zinamapungufu

"Timu inapaswa kusajili wachezaji wazuri kulingana na mapungufu yaliyopo kikosini na sio kusajili wachezaji wengi ambao hawana msaada kwenye timu" alisema.

Bingwa na mshindi wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara moja kwa moja watacheza Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) wakati mshindi wa tatu na bingwa wa Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup ( ASFC) watacheza Kombe la Shirikisho.

Hatua ya raundi ya awali itachezwa kati ya Septemba 10-12, 2021, huku marudiano ni kati ya Septemba 17-19, 2021 na hatua ya makundi itachezwa kati ya Februari 11-13, 2022.

Nafasi hizo zimepatikana baada ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizokusanya alama nyingi zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Mpira wa Miguu  Afrika (CAF).