Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Uhamiaji auona Ubingwa ZPL

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, Ikram ambaye amejiunga na timu hiyo msimu huu, amesema anaona Uhamiaji ipo katika njia nzuri ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar licha ya uwepo wa ushindani mkubwa.

KIUNGO mkabaji wa Uhamiaji, Ikram Said Ally amesema uwepo wake ndani ya kikosi hicho ni miongoni mwa mafanikio makubwa kwani ndiyo mara ya kwanza kucheza  Ligi Kuu Zanzibar.

Hata hivyo, Ikram ambaye amejiunga na timu hiyo msimu huu, amesema anaona Uhamiaji ipo katika njia nzuri ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar licha ya uwepo wa ushindani mkubwa.

“Msimu huu Uhamiaji FC naiona mbali na pia naamini tutafanya vizuri na kuchukua ubingwa tukiendelea kushirikiana na wachezaji wenzangu, bechi la ufundi na viongozi tutachukua ubingwa,” amesema.

Uhamiaji katika mechi nne za Ligi Kuu Zanzibar msimu huu imeshinda zote ikiongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 12, ikifunga mabao tisa na kuruhusu moja.

Kiungo huyo amesema anaamini baada ya miaka michache ijayo anajiona mbali zaidi katika Ligi ya Zanzibar kutokana jitihada anazozifanya, huku akiwasihi vijana wasikate tamaa na kuamini kwamba kila kitu kinawezekana mbele ya Mungu.

“Mal engo yangu zaidi ni kupiga hatua zaidi ya hapa nilipo kwa kucheza ligi kubwa za Afrika na hata nje kwa sababu hiyo ndiyo ndoto yangu ya muda mrefu,” amesema.