Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Polisi autaka Ubingwa ZPL

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Timu ya Polisi itashuka dimbani dhidi ya Black Sailors Oktoba 31, 2026 katika mzunguko wa tisa wa Ligi Kuu Zanzibar katika Uwanja wa Mao B uliopo Unguja.

KIUNGO wa Polisi Zanzibar, Abdul Said Migomba ‘Nyau’ amesema lengo la timu hiyo msimu wa 2026-2027 ni kuandika rekodi mpya ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar.

Timu ya Polisi msimu huu inaonekana kuwa katika kiwango bora kwani mpaka sasa haijapoteza mchezo hata mmoja, ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 18.

Nyau amesema, anaamini kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na kila timu inacheza kwa malengo na tahadhari, hivyo kwa upande wao wanakuwa makini wanaposhuka uwanjani. Amesema msimu huu wanatamani ubingwa wa ligi na hawatanii, akibainisha kwamba wanaodhani wanasindikiza wanajidanganya, hivyo wasubiri waone mwisho wa msimu.

“Nitaipambania timu yangu kila nitakapopata nafasi kuhakikisha inafanya vizuri kila mchezo ili tuweze kutimiza malengo yetu ya kuwa mabingwa,” amesema Nyau. Nyau aliwaomba mashabiki na wapenzi wa timu ya Polisi kuendelea kuwaunga mkono kwani ndiyo kwanza safari imeanza na hawataishia hapo.

Timu ya Polisi itashuka dimbani dhidi ya Black Sailors Oktoba 31, 2026 katika mzunguko wa tisa wa Ligi Kuu Zanzibar katika Uwanja wa Mao B uliopo Unguja.