Beki Muembe Makumbi aitaka nne bora ZPL
Muktasari:
- Muembe Makumbi City inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11, tofauti ya pointi nane na vinara Zimamoto, ambao wamekusanya pointi 19. Akizungumza na Mwanaspoti, Jumbe amesema lengo lao ni kufanya vizuri katika kila mchezo, hatua ambayo wanaamini itawasaidia kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kupanda kwenye msimamo.
BEKI wa Muembe Makumbi City, Jumbe Bakari Washu, amesema licha ya ushindani mkubwa katika Ligi Kuu Zanzibar, lakini kikosi hicho kimejipanga kupambana ili kumaliza msimu kikiwa miongoni mwa timu nne bora.
Muembe Makumbi City inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11, tofauti ya pointi nane na vinara Zimamoto, ambao wamekusanya pointi 19. Akizungumza na Mwanaspoti, Jumbe amesema lengo lao ni kufanya vizuri katika kila mchezo, hatua ambayo wanaamini itawasaidia kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kupanda kwenye msimamo.
Amesema kikosi hicho kitatumia michezo saba iliyosalia kukamilisha mzunguko wa kwanza kuongeza pointi na kujaribu kuingia katika nne bora kabla ya kuweka mikakati mipya kwa hatua inayofuata ya ligi.
“Bila shaka sisi Muembe Makumbi City tunaweza kuwa mabingwa wa ligi kama tutashinda michezo yetu iliyobaki. Tusipofanya hivyo, itakuwa ngumu,” amesema.
Jumbe pia amewaomba mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuendelea kuisapoti katika nyakati zote, akisema sapoti yao itawapa wachezaji nguvu na hamasa ya kupambana zaidi katika michezo ijayo.