Fufuni dakika 720 bila ushindi Ligi Kuu Zanzibar
Muktasari:
- Katika msimu wa 2025-2026, Fufuni ilikuwa miongoni mwa timu zilizofanya vizuri, ikionesha ushindani na kumaliza ligi katika nafasi ya sita. Hata hivyo, hali imebadilika msimu huu wa 2026-2027, huku timu hiyo ikikumbana na matokeo mabaya tangu kuanza kwa ligi.
TIMU ya Fufuni imecheza kwa dakika 720 sawa na mechi nane katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu huu 2026-2027 bila kupata ushindi, ikikusanya pointi mbili na kujikuta mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.
Katika msimu wa 2025-2026, Fufuni ilikuwa miongoni mwa timu zilizofanya vizuri, ikionesha ushindani na kumaliza ligi katika nafasi ya sita. Hata hivyo, hali imebadilika msimu huu wa 2026-2027, huku timu hiyo ikikumbana na matokeo mabaya tangu kuanza kwa ligi.
Katika mechi zake nane ilizocheza, Fufuni imepoteza sita na sare mbili, imefunga mabao matatu na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 12. Matokeo ya mechi ilizofungwa ni bao 1-0 dhidi ya Chipukizi, Wembe (1-0), Polisi (2-1), KVZ (3-0), Uhamiaji (2-1) na Muembe Makumbi (1-0).
Sare ilikuwa bila kufungana dhidi ya Raskazone na mabao 2-2 dhidi ya Black Sailors. Mbali na kukosa ushindi, Fufuni ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi katika mechi hizo nane, ikifuatiwa na Black Sailors iliyofungwa mabao 11.
Kwa mwenendo huo, Fufuni bado haijaonja ladha ya ushindi katika msimu huu wa Ligi Kuu Zanzibar, hali inayoiweka katika wakati mgumu wa kujinasua kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.