Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo aishika pabaya Simba

KIUNGO Pict


HATIMA ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Neo Maema kuendelea kubakia ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2026-2027, iko shakani kutokana na kutofikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya, licha ya kupendekezwa na Kocha Mkuu, Steve Barker.


Nyota huyo aliyechangia Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano 2026 na Kombe la CRDB kwa msimu wa 2025-2026, tayari amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliousaini Agosti 21, 2025, akitokea Mamelodi Sundowns ya kwao Afrika Kusini.


Maema alijiunga na Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Mamelodi Sundowns na kuonyesha kiwango kizuri akiwa na kikosi hicho cha mitaa ya Msimbazi, ingawa kwa sasa mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya yameonekana magumu pande mbili.

Mwanaspoti linatambua vigogo wa timu hiyo walikuwa hawana mpango wa kumwongezea mkataba mpya na badala yake walikuwa pia tayari kutafuta mchezaji mwingine mwenye uwezo mkubwa, japo Kocha, Steve Barker alimpendekeza aendelee kubakia kikosini.

KIUNG 01

Sababu za Barker kutaka nyota huyo kuendelea kubakia kikosini ni kutokana na kiwango bora alichokionyesha katika mechi za mashindano mbalimbali ya kikosi hicho kwa msimu wa 2025-2026, japo matumaini ya kubakia kwake kwa sasa yako shakani.

Chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Simba, kimeliambia Mwanaspoti mustakabali wa nyota huyo kubakia ni mdogo zaidi baada ya kutaka kuongezewa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na mwanzoni, jambo ambalo huenda likachangia akaondoka kikosini.

"Kocha alionyesha imani kubwa kwake na alitaka aongezewe mkataba mpya ila lilipokuja suala la majadiliano ndipo ikawa ni ngumu kwa pande zote mbili kuafikiana, japo mazungumzo bado yanaendelea na hayajafikia mwishoni," kilisema chanzo hicho.

KIUNG 02

Chanzo hicho kililiambia Mwanaspoti, mbali na kutaka kuongezewa mshahara ila mchezaji huyo alitaka kupewa mkataba pia wa miaka miwili, japo uongozi ulikuwa unafikiria kumpa mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine ikiwa wataridhika naye.

Ugumu wa nyota huyo kubakia kwenye timu hiyo ulichagizwa na kutoonekana kwake katika kikosi kilichoenda Rwanda kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Kagame 2026, huku taarifa zikidai bado yupo kwao Afrika Kusini akisubiri kujua mustakabali wake.

Mbali na kuiwezesha pia Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano 2026 na Kombe la CRDB kwa msimu wa 2025-2026, Neo Maema alihusika na mabao matano ya Ligi Kuu Bara kwa msimu mzima wa 2025-2026, baada ya kufunga moja na kuasisti manne.

KIUNG 03

Licha ya kuichezea Mamelodi Sundowns na Simba, mchezaji huyo amecheza pia timu mbalimbali zikiwemo Royal AM FC Reserves kuanzia za vijana hadi za wakubwa, akiwa ni miongoni mwa nyota wa kigeni waliofanya vizuri msimu wa 2025-2026.