Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajuna azikwa Dar, aacha pengo Simba

MAZIKO Pict

Muktasari:

  • Kajuna aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Julai 23, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Moyo, alikuwa amepumzishwa hospitalini hapo kwa takribani siku saba kabla ya kufikwa na umauti.

ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Idd Kajuna, amezikwa jioni ya jana Julai 23, 2026 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, huku wadau mbalimbali wa soka na viongozi wa Simba wakisema ameacha pengo klabuni hapo.

Kajuna aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Julai 23, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Moyo, alikuwa amepumzishwa hospitalini hapo kwa takribani siku saba kabla ya kufikwa na umauti.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori, amesema Simba imepoteza mpambanaji jasiri wa klabu hiyo.

Magori amesema Kajuna hakuwa tu kiongozi, bali alikuwa tayari wakati wote kuipigania Simba hata kabla ya kuteuliwa kwenye kamati hiyo.

"Hizi ni taarifa mbaya sana kwa Simba, tumepoteza mtu wa kupigana vitani, ni msiba mkubwa ndani ya Simba, alikuwa tayari wakati wote kuipambania Simba yake," amesema Magori.

"Unaweza kusema labda kwa sababu alikuwa kiongozi, lakini hapana, alikuwa anaipigania klabu hii hata kabla ya kuwa kiongozi na hilo ndilo likatufanya kumchagua kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano."

Kajuna aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba mwaka jana na amehudumu kwenye nafasi hiyo hadi umauti unamkuta huku kazi yake ya mwisho ikiwa ni Fainali ya Kombe la CRDB iliyofanyika kisiwani Pemba Julai 4, 2026 na Simba kuwa bingwa ikiifunga Azam bao 1-0.

Kajuna pia alikua Mjumbe wa Baraza la ushauri lilioundwa na Rais wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji. Kabla ya hapo Kajuna amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba mwaka 2017 na Mjumbe wa kamati ya utendaji kuanzia mwaka 2014 hadi 2018.

Kajuna pia amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya mpito ya Wakurugenzi mwaka 2018 wakati wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uongozi.

"Uongozi wa klabu unaungana na familia, ndugu, jamaa na Wanamichezo wote kuomboleza msiba huu wa Mwanasimba mwenzetu na tunaiombea kwa Mwenyezi Mungu roho yake ipumzike salama," ilisema taarifa ya Klabu ya Simba.