Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa ukata Tanzania yajitoa kikapu Afrika

Kisa ukata Tanzania yajitoa kikapu Afrika

Muktasari:

  • Nchi nyingine inazoshiriki kwenye mshindanohayo ni Misri, Senegal, Mali, Benin, Guinea, Angola, Rwanda, Algeria na wenyeji Madagascar.

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limeeleza kuitoa timu ya wavulana kushiriki mashindano ya Afrika ya kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 18.

Taarifa ya TBF inasema, timu hiyo sasa haitashiriki kwenye mashindano hayo ya siku 10 yatakayofunguliwa Agosti 4 nchini Madagascar kutokana na ukata.

"Shirikisho limekosa pesa za kuipeleka timu ya wavulana, hivyo msimu huu tutawakilishwa na timu ya wasichana pekee," ilisema taarifa ya TBF.

Taarifa hiyo ilisema Tanzania ilipata uwakilishi wa timu mbili ya wavulana na wasichana kwenye mashindano hayo yanafanyika kulingana na kalenda ya Shirikisho la kikapu Afrika (FIBA Afrika).

Timu zitakazofanya vizuri kwenye mashindano hayo zitaliwakilisha bara la Afrika kwenye mashindanoya dunia baadae mwakani nchini Hungary.

"Timu yetuya taifa ya wavulana haitakwenda kutokana na kukosa fedha, ingawa uamuzi huu umezingatia muda wa kuthibitisha ili kuepusha adhabu ya kujitoadhidi yetu japo utaathiri viwango vya nchi ambavyo hutegemea ushiriki kimataifa wa timu zetu," imesema taarifa hiyo.