Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa dabi, kikao kizito Yanga

YANGA Pict

Muktasari:

  • Kabla ya dabi hiyo ambayo inahitimisha rasmi msimu wa mashindano hayo, ilitawaliwa na kaulimbiu ya HATUCHEZI iliyogonga vichwa vya habari na kushika kasi mitaani ambako mashabiki wa Yanga walitamba nayo dhidi ya wapinzani wao, kwamba mechi ya dabi ya pili ya ligi msimu huu wasingecheza.

WABABE wa soka la Bongo, Simba na Yanga wanakutana kesho katika mechi ya Dabi ya Kariakoo ambayo imetawaliwa na mambo kibao na ambayo imekuwa ikitembea kwa muda mrefu na kaulimbiu moja kwa muda mrefu kabla ya kuamriwa kwamba itapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


Kabla ya dabi hiyo ambayo inahitimisha rasmi msimu wa mashindano hayo, ilitawaliwa na kaulimbiu ya HATUCHEZI iliyogonga vichwa vya habari na kushika kasi mitaani ambako mashabiki wa Yanga walitamba nayo dhidi ya wapinzani wao, kwamba mechi ya dabi ya pili ya ligi msimu huu wasingecheza.


Lakini, mambo yamegeuka na sasa chama hilo la Jangwani limekubali kukabiliana na watani zao, keshokutwa, huku vita ikitarajiwa kuwa ya aina yake kombe la ubingwa likiwa pale mezani. 

Wakati mambo yakiwa hivyo, Yanga inacheza Dabi ya Kariakoo Juni 25, na kuthibitisha hilo kuna kikao kizito kimefanyika Zanzibar kikiwa ni maalum kwa ajili ya mchezo huo huku viongozi wa klabu hiyo wakitamka na kutoa msimamo wao.

Jana Jumatatu kikosi cha Yanga kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, kilifanyika kikao kizito kilichowahusisha wachezaji, viongozi wa benchi la ufundi na mabosi wa juu wa timu hiyo kisha kuweka msimamo mkali wa kutafuta ushindi kwenye mchezo huo.

Yanga itakutana na Simba kwenye mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Bara ulioahirishwa mara mbili kutoka Machi 8, 2025 kisha Juni 15, 2025 na sasa utapigwa Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mabosi wa Yanga wamewataka wachezaji wa timu hiyo kurudisha utulivu wa akili yao kuelekea mchezo huo, wakiipa jina kwamba mchezo huo umebeba heshima ya viongozi wao na mashabiki wao.

Ndani ya kikao hicho, mabosi hao wamewataka wachezaji kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe wakati wa maandalizi ya mwisho ambapo kitu pekee kinachohitajika ni ushindi na matokeo ya mwisho yawe sare.

"Tumekutana na vijana tumewaambia maana halisi ya mchezo huu, inawezekana kwamba wamecheza mechi nyingi lakini hivi karibuni hatukuwahi kuwa na mchezo dhidi ya Simba kwenye ligi ambao unakwenda kutoa uamuzi wa nani anakuwa bingwa," amesema bosi huyo.

"Tunataka ushindi kwenye mechi hii, kuna matokeo mawili tu kushinda na ya mwisho kabisa kupata sare na sio kingine, tuna kikosi imara ambacho kinaweza kutupa matokeo tunayoyataka."

Baada ya kikao hicho, mastaa wa timu hiyo nao wakatoa msimamo wao wakiwaambia mabosi kuwa wanautaka mchezo huo ili kutoa heshima kwa mashabiki wao.

Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam jana mchana tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 11 jioni.

Yanga inataka ushindi au sare kujihakikishia ubingwa wa ligi msimu huu kwa mara ya nne mfululizo wakati watani wao Simba wakiwa na hitaji moja tu la kushinda ili kuwa mabingwa.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga inaongoza ikiwa na pointi 79, inafuatiwa na Simba yenye 78, zote zikicheza mechi 29, tofauti ya pointi moja ndiyo inawatenganisha wakongwe hao wa soka Tanzania Bara.