Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo chamuibua Kocha Mlandege

MLANDEGE

Muktasari:

  • Mlandege ilipokea kichapo hicho kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ, mechi iliyochezwa Septemba 23, 2026 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

KOCHA Msaidizi wa Mlandege, Sabri China amesema makosa yaliyofanya na wachezaji wa timu hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya kupoteza mechi yao ya Ligi Kuu Zanzibar kwa mabao 2-0 dhidi ya KVZ.

Mlandege ilipokea kichapo hicho kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ, mechi iliyochezwa Septemba 23, 2026 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Mabao ya KVZ yalifungwa na kiungo, Yakoub Said dakika ya sita na mshambuliaji Akram Muhina ‘Haaland’ dakika ya 87.

Kocha huyo amesema, bao la kwanza waliloruhusu lilitokana na beki wa timu hiyo akiwa katika nafasi nzuri ya kumiliki mpira, mpinzani alikuwa tayari amefika eneo la hatari na kufunga.

“Tunafungwa kwa sababu ya wachezaji kutokuwa makini ingawa tunajitahidi kuwaweka sawa kisaikolojia lakini bado wanarudia makosa yanayoigharimu timu,” amesema.

Pia, amesema mawinga ambao wana jukuma la kuis ogeza timu mbele kushambulia walikuwa hawachezi kwenye kiwango chao cha kawaida. “Kufungwa na KVZ ni jambo ambalo linatuuma sana hadi sasa na tukiangalia hatupo katika hali nzuri,” amesema.

Timu ya Mlandege haina mfululizo matokeo mazuri  kwenye ligi hiyo ambapo hadi sasa katika mechi sita ilizocheza, imeshinda moja, sare mbili na kupoteza tatu, ikikusanya pointi tano, ikiwa nafasi ya kumi kabla ya mechi za jana.