Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Singida arejea Nigeria

Muktasari:

  • Kipa huyo aliyejiunga na Singida katika dirisha dogo la Januari 2025, baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa na kikosi cha Fasil Kenema ya Ethiopia, alisaini mkataba wa miaka miwili, ingawa ameitumikia kwa mwaka mmoja na nusu.

ALIYEKUWA kipa wa Singida Black Stars, Mnigeria, Amas Obasogie amefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea na timu hiyo kwa msimu wa 2026-2027, licha ya kubakisha mkataba wa miezi sita uliokuwa unafikia tamati Desemba 2026.

Kipa huyo aliyejiunga na Singida katika dirisha dogo la Januari 2025, baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa na kikosi cha Fasil Kenema ya Ethiopia, alisaini mkataba wa miaka miwili, ingawa ameitumikia kwa mwaka mmoja na nusu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Obasogie alisema amefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuachana na timu hiyo, ambapo tayari ameanza mazungumzo na klabu mbalimbali, ikiwemo Bendel Insurance FC ya kwao Nigeria aliyowahi kuichezea.

“Hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na timu mpya nitakayocheza msimu wa 2026-2027, ila kuhusu nafasi yangu Singida haipo tena kwa sababu nimeachana nao kwa amani, malengo yangu ni kupata changamoto sehemu nyingine,” alisema Obasogie.

Katika msimu wake wa kwanza wa 2024-2025, akiwa na kikosi hicho cha Singida Black Stars, alimaliza na clean sheets sita za Ligi Kuu Bara, nyuma ya mzawa, Metacha Mnata anayeendelea kucheza timu hiyo aliyemaliza akiwa na saba.

Msimu wa 2025-2026, kipa huyo alikuwa na clean sheets nne za Ligi Kuu Bara, nyuma ya Metacha aliyeongoza pia akiwa na tano, ambapo nafasi yake ameongezwa Yona Amos aliyeachana na kikosi cha Pamba Jiji, baada ya mkataba wake kumalizika.

Amos aliyemaliza msimu wa 2025-2026 na clean sheets nane za Ligi Kuu akiwa na kikosi hicho cha Pamba Jiji, ni miongoni mwa kipa mzawa bora kwa sasa, anayetarajiwa kuongeza ushindani zaidi kwa Metacha.