Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mangalo suala la muda Mashujaa

Muktasari:

  • Usajili wake ukikamilika, Mangalo ataungana na wachezaji wengine wapya ndani ya kikosi hicho, miongoni mwao ni kiungo mshambuliaji Hassan Kabunda kutoka Namungo na beki wa kati Abdallah Mfuko aliyetokea pia Namungo.

MASHUJAA ipo hatua ya mwisho kukamilisha usajili wa beki, Abdulmajid Mangalo kutoka Pamba Jiji, kuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu ujao unaotarajia kuanza Agosti 14,2026.

Usajili wake ukikamilika, Mangalo ataungana na wachezaji wengine wapya ndani ya kikosi hicho, miongoni mwao ni kiungo mshambuliaji Hassan Kabunda kutoka Namungo na beki wa kati Abdallah Mfuko aliyetokea pia Namungo.

Kigogo mmoja wa Mashujaa, aliliambia Mwanaspoti kwamba wamebakiza vitu vichache kumalizana na Mangalo wanayeamini ataongeza nguvu na ushindani katika kikosi hicho. “Tumesajili wachezaji wengi, lakini tutawatangaza kwa utaratibu tuliojiwekea kama timu. Kuhusu Mangalo tuna asilimia 99 atakuwa sehmu ya kikosi chetu,” alisema kigogo huyo na kuongeza;

“Mashujaa tumefanya mabadiliko kiasi ya kikosi, jambo la msingi hatuhitaji msimu ujao kupambana ili timu isishuke daraja, bali tupambanie nafasi za juu, ndiyo maana tumefanya marekebisho ya kile tunachoamini kitasaidia kukamilisha malengo yetu.”

Mbali na usajili wa wachezaji, timu hiyo imefanya maboresho ya benchi la ufundi ambapo sasa itafundishwa na Aman Josiah aliyetokea Dodoma Jiji, baada ya kuachana na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.