Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KVZ yaondoshwa Cecafa Kagame Cup

Muktasari:

  • Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa KVZ baada ya kuanza michuano hiyo kwa kufungwa mabao 2-0 na Rayon Sports ya Rwanda.

KVZ ya Zanzibar imeaga mashindano ya Kombe la CECAFA Kagame baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa Kundi C uliochezwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele, Rwanda.

Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa KVZ baada ya kuanza michuano hiyo kwa kufungwa mabao 2-0 na Rayon Sports ya Rwanda.

Al Hilal ilianza mchezo kwa kasi na kupata bao la mapema dakika ya tano kupitia mshambuliaji Mohamed Abdelrahman, kabla ya Ahmed M'Bracek kuongeza la pili dakika ya 29 na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili, KVZ ilijaribu kubadilisha mchezo, lakini ilishindwa kuhimili presha ya wapinzani wake. Ansumana Samura aliifungia Al Hilal bao la tatu dakika ya 81, kabla ya Taiwo Akire kuhitimisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne katika dakika ya 91.

Matokeo hayo yameifanya KVZ kubaki mkiani mwa Kundi C bila pointi, ikiwa tayari imeruhusu mabao sita katika mechi mbili huku ikishindwa hata kupata bao.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, vinara wa makundi matatu watafuzu moja kwa moja kwenda nusu fainali, huku nafasi ya nne ikichukuliwa na timu itakayomaliza ya pili ikiwa na matokeo bora zaidi ya nyingine.

Mbio za nafasi ya timu bora ya pili pia zinaendelea katika Kundi B, ambako Simba yenye pointi mbili bado ina matumaini ya kufuzu endapo itaifunga Singida Black Stars katika mchezo wake wa mwisho, huku ikisubiri matokeo ya mechi nyingine.

Vipers SC ya Uganda tayari imekata tiketi ya nusu fainali kutoka Kundi A baada ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo na kufikisha pointi sita, ikithibitisha ubora wake katika michuano ya mwaka huu.