Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Mmalawi atua kukipiga Mbeya City

KIPA Pict

Muktasari:

  • Usajili huo ni mwendelezo wa kusuka upya timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya, huku ikiwa imemalizana pia na mastaa wengine akiwamo Jimmyson Mwanuke, Omary Buzungu na kipa Toba Kutisha.

WAKATI Mbeya City ikiendelea kujifua huko Mwakaleli kujiandaa na Ligi Kuu Bara msimu ujao, imefanya kweli kwa kumshusha kikosini Kipa wa kimataifa kutoka Malawi, Brighton Munthali kuwatumikia wababe hao wa jijini Mbeya.

Usajili huo ni mwendelezo wa kusuka upya timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya, huku ikiwa imemalizana pia na mastaa wengine akiwamo Jimmyson Mwanuke, Omary Buzungu na kipa Toba Kutisha.

Munthali (28) ametua kikosini humo kwa kandarasi ya miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Blue Eagles ya Malawi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Mbeya City, Gwamaka Mwankota amesema usajili huo si mwisho bali ipo ‘surprise’ nyingine kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Agosti 15, 2026.

Amesema wakati wakiendelea kujifua kambini Mwakaleli, benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Salum Mayanga wamepanga kucheza mechi nne za kirafiki ikiwa ni kujaribu ubora wa nyota wake.

“Tunaahidi msimu ujao kutoa burudani kwa mashabiki wetu, hatutarajii tena presha zilizotokea msimu uliopita, ndiyo maana tunafanya usajili bora, maandalizi mazuri ili kuja kwa nguvu mpya msimu ujao.

“Katika mechi hizo za kirafiki tutacheza mbili nyepesi na nyingine ngumu za ushindani ili kujaribu silaha zetu kabla ya kushuka uwanjani Agosti 14 kuwakabili Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu,” amesema Mwankota.

Kuhusu tamasha la Mbeya City Day ambalo hulifanya kila msimu, Mwankota amesema msimu huu hakutakuwapo tukio hilo kutokana na kubana kwa muda, akieleza kuwa usajili na mipango ya jumla wataitangaza kivingine.