Kipanga ipo tayari kwa msimu mpya
Muktasari:
- Amesema wanatarajia msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa kuliko uliopita na kuvutia kwa sababu timu nyingi zimeboresha vikosi vyao , lakini hilo haliwatishi kwani nao wamejipanga vizuri.
IKIWA zimebaki siku chache kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Zanzibar, Kocha wa Kipanga, Khamis Hassan Makame 'Kocha Meki' amesema wapo tayari kwa ajili ya mapambano..
Amesema mikakati yao ni kukamilisha malengo yao ambayo wameshindwa kuyatimiza msimu uliopita ndiyo maana wamefanyia maboresho kikosi chao kwa asilimia kubwa.
Ligi hiyo inatarajiwa kuanza Agosti 29, 2026 huku mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya KVZ na KMKM ukichezwa Agosti 23.
Katika kufikia hayo, Kocha Meki amesema wanaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mtoni, hadi kufikia sasa timu ipo vizuri na kuimarika na inaendelea vizuri huku timu ikiimarika kila siku.
"Wachezaji wetu wengi wamesharipoti kambini ingawa kuna baadhi yao wachache bado hawajaripoti lakini nategemea kuanzia wiki ijayo wote watakuwa wameshafika na kujiunga na wenzao," amesema
Amesema wanatarajia msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa kuliko uliopita na kuvutia kwa sababu timu nyingi zimeboresha vikosi vyao , lakini hilo haliwatishi kwani nao wamejipanga vizuri.