Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibarua cha kwanza cha Edna Lema

EDNA Pict

Muktasari:

  • Edna, aliyetambulishwa ndani ya kikosi cha Mashujaa Novemba 10, 2026, akisaini mkataba wa mwaka mmoja, sasa anakabiliwa na mtihani wake wa kwanza akiwa na jukumu la kuanza kujenga timu hiyo kwa kuzingatia falsafa yake ya soka.

Baada ya kuachana na Yanga Princess na kujiunga na Mashujaa Queens, kocha Edna Lema anatarajiwa kuanza rasmi kibarua chake kipya Novemba 18 mwaka huu, atakapokiongoza kikosi hicho kuvaana na Tausi FC.

Edna, aliyetambulishwa ndani ya kikosi cha Mashujaa Novemba 10, 2026, akisaini mkataba wa mwaka mmoja, sasa anakabiliwa na mtihani wake wa kwanza akiwa na jukumu la kuanza kujenga timu hiyo kwa kuzingatia falsafa yake ya soka.

Kocha huyo aliondoka Yanga Princess baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na Simba Queens katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Septemba 30 mwaka huu.

ED 01

Hata hivyo, mtihani wake wa kwanza akiwa Mashujaa unamkutanisha na mpinzani anayemfahamu vizuri kutokana na historia ya kukutana naye akiwa akiinoa Yanga Princess.

Katika michezo miwili ya msimu uliopita dhidi ya Tausi FC, Edna aliambulia pointi tatu kati ya sita, akipata ushindi mmoja na kupoteza mchezo mwingine.

Desemba 12, 2025, Yanga Princess ikiwa chini ya Edna iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tausi, lakini Aprili 8, 2026, ilijikuta ikipoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Azam Complex.

Safari hii anakutana na Tausi FC inayohitaji kujinasua baada ya kuanza vibaya msimu wa 2026/27, ikiwa imepoteza mechi zote tatu za mwanzo.

ED 02

Tausi ilianza kwa kufungwa mabao 5-2 na Bunda Queens, kabla ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Alliance Girls na baadaye kuchapwa mabao 2-0 na Ceasiaa Queens.

Akizungumzia matarajio yake ndani ya klabu hiyo mpya, Edna amesema anatamani kuiona Mashujaa ikifanya vizuri, huku akilenga kujenga kikosi kitakachocheza soka la ushindani na kuvutia mashabiki.

“Natamani kuiona Mashujaa inafanya vizuri, natamani kuiona falsafa yangu inakubalika na watu wakisikia timu inacheza waje uwanjani kwa sababu mimi ni kocha ninayependa ushindani,” amesema Edna.