Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibano kwa makocha sita Ligi Kuu

MAKOCHA Pict

Muktasari:

  • Hii ni baada ya timu hizo kupoteza na kuambulia sare na kuwa nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, hali inayoongeza joto kali kwa mashabiki na wadau wa timu hizo katika vita ya kupambana kukwepa aibu ya kushuka daraja.

MATOKEO ya mechi zilizopita yameonekana kuwaweka kikaangoni makocha sita kufuatia mwenendo usioridhisha na kuhatarisha vibarua vyao kutokana na presha ya kukwepa kushuka daraja msimu huu.

Hii ni baada ya timu hizo kupoteza na kuambulia sare na kuwa nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, hali inayoongeza joto kali kwa mashabiki na wadau wa timu hizo katika vita ya kupambana kukwepa aibu ya kushuka daraja.

Makocha hao ni Fredi Felix ‘Minziro’ (Fountain Gate), Cedrick Kaze (Kagera Sugar), Francis Baraza (Pamba Jiji), Hemed Suleiman ‘Morocco’ (TRA United), Zuberi Katwila (Geita Gold) na Salum Mayanga (Mbeya City).

Minziro ameanza msimu na timu hiyo ambapo bado hajawa na matokeo mazuri, akishinda mchezo mmoja, huku Kaze aliyechukua nafasi ya Juma Kaseja, akishinda mmoja kati ya minne aliyoongoza.

MAKO 01

Baraza raia wa Kenya naye hali imekuwa tete msimu huu baada ya kupata ushindi mmoja kwenye michezo 10 aliyosimamia Pamba Jiji, wakati Morocco wa TRA United aliyerithi mikoba ya Ettiene Ndayiragije akishinda mmoja kati ya minne, akipoteza mmoja na sare mbili.

Katwila ambaye ameipandisha Geita Gold, ameshinda michezo miwili kati ya 10 aliyoongoza, ilhali Mayanga akiambulia ushindi michezo mitatu kwa Mbeya City kati ya tisa aliyosimamia tangu msimu kuanza.

Katika mechi zilizopita, Fountain Gate ililala bao 1-0 dhidi ya Simba na kufikisha michezo nane bila ushindi ikiwa ni sare tatu na kupoteza mitano, ipo mkiani kwa pointi sita baada ya kucheza mechi 10.

MAKO 02

Kwa upande wa Kagera Sugar ilipoteza dhidi ya Coastal Union bao 1-0 na kuwa mchezo wa tatu kukosa ushindi ikiwa ni sare moja na kupoteza miwili na kuwa nafasi ya 15 kwa pointi sita ikicheza mechi 10.

Geita Gold iliyopo nafasi ya 14, iliambulia sare ugenini ya 1-1 dhidi ya TRA United na kufikisha saba mfululizo bila ushindi ikiwa ni sare tatu na kupoteza minne.

Mbeya City ambao ni wawakilishi pekee Nyanda za Juu Kusini, kipigo cha 4-0 kinafikisha mechi sita mfululizo bila kuonja pointi tatu ikiwa ni sare mbili na kupoteza minne na kuwa nafasi ya 11 kwa pointi 10.

MAKO 03

Mchambuzi wa soka jijini Mbeya na nyota wa zamani wa Tukuyu Stars na Coastal Union, Charles Makwaza, amesema mapumziko ya kupisha kalenda ya FIFA kuna namna imezipunguza kasi timu hizo.

Amesema awali baadhi ya timu hizo ikiwamo Mbeya City na Geita Gold zilikuwa na mwanzo mzuri na kutabiriwa makubwa lakini kwa sasa zinaanza kuombewa dua kuepukana na lolote huko mbeleni.

“Inahitaji juhudi za haraka na makusudi kwa viongozi wa hizo timu kukaa na wachezaji kujua wanatokaje, mfano Nyanda za Juu Kusini tunaitegemea sana Mbeya City, lazima kuwapo na jitihada maalumu,” amesema mkongwe huyo.