Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katwila mambo safi Geita Gold

KATWILA Pict

Muktasari:

  • Kikao hicho kilikuja wakati ambao Geita Gold inapitia wakati mgumu jambo lililoongeza presha kwa Katwila baada ya kupoteza mechi tano kati ya nane msimu huu. Hata hivyo, badala ya kukimbilia kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi, uongozi umeamua kutafuta suluhisho la changamoto zilizokuwa zimejitokeza ndani ya timu.

GEITA Gold imeamua kuweka pembeni sintofahamu zilizokuwa zikiizunguka baada ya kikao kizito kilichowakutanisha wachezaji, benchi la ufundi na bodi ya klabu, huku kocha Zuberi Katwila akihakikishiwa kuendelea na kazi ili kurejesha makali ya timu Ligi Kuu Bara.

Kikao hicho kilikuja wakati ambao Geita Gold inapitia wakati mgumu jambo lililoongeza presha kwa Katwila baada ya kupoteza mechi tano kati ya nane msimu huu. Hata hivyo, badala ya kukimbilia kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi, uongozi umeamua kutafuta suluhisho la changamoto zilizokuwa zimejitokeza ndani ya timu.

Taarifa za ndani zilidai kikao hicho kililenga kuweka sawa sintofahamu zilizokuwa zimeibuka baina ya pande zinazohusika na uendeshaji wa timu hiyo na benchi la ufundi, huku kila upande ukipata nafasi ya kueleza changamoto zake na namna unavyoona mambo yanavyopaswa kwenda kuanzia sasa.

“Baada ya mazungumzo tuliyoyafanya na wachezaji, benchi la ufundi kama uongozi tumekubaliana kuweka nguvu zetu pamoja na kupambana kutafuta matokeo mazuri katika mechi zinazofuata, “ kilisema chanzo hicho.

Rekodi zinaonyesha katika mechi nane timu hiyo ilikuwa imeshinda mara mbili, sare moja na kupoteza tano, huku ikifunga mabao 10 na kuruhusu 16. Mechi ijayo Geita itakutana na Fountain Gate,  Uwanja wa Kwaraa, Babati.