Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

John Terry alivyorithi tabia mbovu za wazazi wake

Muktasari:

  • Julai mwaka huu, katika tukio moja la kushangaza, mama yake Terry, Sue alienda kujirusha na mkwewe Toni (mke wa Terry) katika klabu moja ya usiku jijini London.

LONDON, ENGLAND

JOHN Terry anapokea mshahara wa Pauni 150,00 kwa wiki, lakini juzi baba yake ameshindwa kuajiri wakili wa kumtetea kwa gharama za Pauni 340 tu. Hizi zote ni laana za familia yake ambayo imeoza kwa maovu nchini England.

Mama yake John Terry ni kibaka, baba yake ni muuza unga, wakati kaka yake amewahi kusababisha kifo cha mwanasoka mwenzake kwa wivu wa mapenzi.

Mama yake aiba dukani

Machi 27, 2009, katika kashfa ya kushangaza, mama yake John Terry, Sue Terry na mkwe wa John Terry (mama wa mkewe) aliyefahamika kwa jina la Sue Pool, walikutwa na vitu vya wizi ambavyo hawajalipia katika maduka ya Tesco na Mark & Spencer mjini Surrey.

Kilichowashangaza wafanyakazi wa duka hilo ni jinsi kinamama hao wawili walivyokuwa bize kupakia mizigo hiyo katika gari huku ikiwa haijalipiwa.

Vitu vyote hivyo vilikuwa na thamani ya Pauni 800 na walipohojiwa na polisi baadaye  walisingizia kwamba walikuwa hawana uhakika kama hawajalipa. Hata hivyo walikuwa na aibu isiyo na kifani katika sura zao.

Mama alewa alala nusu uchi

Julai mwaka huu, katika tukio moja la kushangaza, mama yake Terry, Sue alienda kujirusha na mkwewe Toni (mke wa Terry) katika klabu moja ya usiku jijini London.

Hata hivyo, mama huyo alilewa chakari na kuamua kwenda moja kwa moja katika teksi iliyokuwa nje inawasubiri huku akimwacha Toni ndani. Aliingia katika teksi na kulala siti ya nyuma huku akiwa amefunua mapaja yake.

“Ndani ya ukumbi Sue alikuwa kila mahala. Alionekana yuko katika matatizo kutokana na ulevi mwingi kichwani. Nadhani alikuwa amekunywa sana. Alikuja nje nusu saa kabla ya Toni. Alienda moja kwa moja katika siti ya nyuma na kulala,” anasema shuhuda mmoja aliyekuwa karibu nao.

Kumbe tabia za John Terry katika ulevi ni kama za kurithi tu. Septemba 12, 2001 ikiwa ni siku moja tu baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 12, 2001, Terry alikuwa miongoni mwa wachezaji wanne chipukizi walioamua kufanya matanuzi ya kilevi katika baa mbalimbali za Jiji la London.

Moja kati ya baa walizokwenda ni katika hoteli ya Uwanja wa Ndege wa Heathrow ambapo waliwakuta wasafiri kibao raia wa Marekani waliokuwa wanafuatilia kwa karibu mashambulizi hayo ya kigaidi kupitia televisheni.

Tabia yao iliwakera watu waliokuwa karibu yao na taarifa zilifika katika klabu ya Chelsea huku wote wakipigwa faini kama adhabu.

Kaka asababisha kifo

Desemba 2010, kipa wa klabu ya Rushden & Diamonds, Dale Roberts alijiua katika kile kilichosadikika kuwa wivu wa mapenzi. Alijiua katika nyumba aliyokuwa anaishi na mpenzi wake Lindsay Cowan iliyopo Higham Ferrers, Northamptonshire.

Uchunguzi wa kipolisi ulionyesha kwamba Dale alijiua baada ya kukumbwa na jinamizi kubwa la wivu wa kimapenzi baada ya penzi lao kuvunjika kwa muda mfupi Mei, 2010 kutokana na mpenzi wake kuwa na uhusiano na kaka yake, John Terry, Paul Terry ambaye alikuwa mchezaji mwenzake.

Baadaye Dale alikataa kucheza na Terry kiasi kwamba wachezaji wenzao walitaka Terry afukuzwe kwa kitendo chake hicho. Baadaye, Lindsey na Roberts walirudiana lakini kamwe Roberts hakuweza kulimudu jinamizi la usaliti alilofanyiwa na Lindsey kiasi cha kuamua kujiua mwenyewe.

Unaitofautishaje habari hii na ile ya John Terry kutembea na mpenzi wa mchezaji mwenzake, Wayne Bridge, Vanessa Perroncel, kiasi cha Terry kuvuliwa unahodha wa timu ya taifa ya England?

Baba auza Cocaine baa

Mwaka 2011, baba yake John Terry, Ted Terry alikutwa akiuza dawa za kulevya aina ya Cocaine katika choo cha baa moja jijini London. Alihukumiwa kifungo cha miezi sita na kufanya kazi za jamii kwa saa 100.

Hata hivyo, alifanikiwa kuepuka kifungo hicho baada ya kujitetea kwamba kosa hilo alikuwa ametegewa na mwandishi wa gazeti moja la udaku.

Baba ampiga na kumbagua mhindi

Wiki chache zilizopita, baba yake Terry, Ted, kwa mara nyingine ameleta kasheshe mpya baada ya kutuhumiwa kumshambulia raia mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Kiasia, Amarjit Talafair jijini London.

Inadaiwa kwamba Ted alimpiga kichwa Talafair katika ugomvi mmoja wa klabu ya usiku. Hata hivyo, mwenyewe anadai kwamba tukio hilo halikutokana na ubaguzi wa rangi kama ilivyoripotiwa ingawa alikubali kwamba alifanya shambulio la mwili.

Unawezaje kutofautisha madai hayo na yale ya mwanaye ambaye inadaiwa alimbagua mlinzi wa QPR, Anton Ferdinand katika pambano la Ligi Kuu misimu miwili iliyopita? Polisi walimsafisha Terry, lakini mabosi wa Ligi Kuu England walimtia hatiani kwa kosa hilo na tangu hapo akatangaza kuachana na timu ya taifa.

Lakini kama ni ugomvi wa disko, basi haukuanzia kwa baba yake. Januari 2002, Terry akiwa na wanasoka wenzake chipukizi, Jody Morris aliyekuwa anakipiga naye Chelsea pamoja na Des Byrne wa Wimbledon walishtakiwa kwa kosa la kumpiga baunsa katika klabu moja ya usiku jijini London.

Katika kipindi cha kesi hiyo, Terry aliondolewa katika orodha ya wachezaji wanaoweza kuchezea timu ya taifa. Hata hivyo baadaye walisafishwa katika kesi hiyo.