Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jezi za kijani na nyeusi zilivyowateka wadada Yanga Day

JEZI Pict

Muktasari:

  • Kilichovuta macho zaidi ni jezi zilizogawanyika kwa mtindo wa nusu goldi na nusu nyeusi, ambazo zimeonekana kuwa chaguo la mashabiki wengi wa kike walioanza kuwasili uwanjani.

UWANJA wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo Agosti 9, 2026 umeonekana kwa na sura tofauti, baada ya mashabiki wa Yanga, hususan wadada, kujitokeza kwa wingi wakiwa wamevalia jezi zenye mchanganyiko wa rangi za kijani na njano.

Kilichovuta macho zaidi ni jezi zilizogawanyika kwa mtindo wa nusu goldi na nusu nyeusi, ambazo zimeonekana kuwa chaguo la mashabiki wengi wa kike walioanza kuwasili uwanjani.

Wadada hao wameonekana wakitembea katika maeneo mbalimbali ya uwanja huku wakiwa wamevalia jezi hizo, jambo lililoongeza mvuto wa tamasha na kufanya rangi za Yanga kutawala katika maeneo ya uwanja.

Mbali na jezi hizo, baadhi ya mashabiki wameonekana wakikamilisha mwonekano wao kwa suruali, kaptula mbalimbali zenye rangi zinazoendana na jezi hizo.

Hali hiyo imeifanya sehemu ya mashabiki wa kike kuwa miongoni mwa waliovuta macho zaidi kabla ya kuanza kwa tamasha la Yanga Day, huku kila mmoja akionekana kufurahia siku hiyo kwa staili yake.