Ishu ya refa Arajiga
SIMBA ina kismati na mwamuzi, Ahmed Arajiga katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam FC (ASFC), ukitofautisha na Yanga.
Arajiga ndiye hakimu wa dabi ya leo Jumamosi ambayo ni mtihani kwake, Yanga ikiwa mwenyeji wa Simba mechi ya nusu fainali ya kusaka tiketi ya kutinga fainali za ASFC.
Rekodi za Arajiga dhidi ya Simba kwenye ASFC ni habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo, vilevile zinaweza kuzua mshtuko kwa wafuasi wa Yanga kwani ndiye aliyekuwa kati fainali ya mwaka jana, iliyopigwa Kigoma.
Mwamuzi wa zamani Mathew Akrama kutoka Mwanza, alisema sheria ni hakimu wa kweli bila kujali matarajio ya mashabiki au ulishawahi kukutana na timu husika mara ngapi uwanjani.
“Kwanza jopo lililomchagua limejua umuhimu wake, ukiachana na hilo mwamuzi anapaswa kusimamia sheria na siyo mashabiki wanataka nini, wachezaji waamue kucheza bila jukwaa, kila kitu kitakaa mahali pake,” alisema.
Mwamuzi mwingine Samwel Mpenzu, alisema anayechezesha anapangwa kulingana na kiwango chake cha kazi.
“Hakuna tatizo kama mwamuzi anafanya kazi yake vizuri kuchezesha mechi nyingi, ukiona hivyo anakuwa ameonyesha kiwango kizuri,” alisema akiongeza kuwa hata akichezesha mechi ngapi mfululizo haina tatizo kitaalam.
Mwanaspoti linakuchambulia rekodi za Arajiga alizoamua mechi za Simba na za Yanga, ikiwemo ile ya Kigoma ambayo Simba iliibuka mabingwa kwa bao la Thadeo Lwanga dakika ya 79.
LIGI KUU MSIMU HUU
Geita 1-1 Simba
Ahmed Arajiga
Yanga 1-0 Geita
Ahmed Arajiga
Yanga 2-1 Namungo
Ahmed Arajiga
Yanga 0-0 Prisons
Ahmed Arajiga
ASFC MSIMU HUU
Ruvu 0-7 Simba
16/02/2022
Hatua ya 16 ASFC
Uwanja wa Mkapa
Refa; Ahmed Arajiga
Simba 4-0 Pamba
14/05/2022
Robo Fainali ASFC
Uwanja wa Mkapa
Refa; Ahmed Arajiga
Yanga v Simba
28/05/2022
Nusu Fainali ASFC
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza
Refa; Ahmed Arajiga
ASFC MSIMU ULIOPITA
Simba 3-0 Dodoma
26/05/2021
Robo Fainali ASFC
Uwanja wa Mkapa
Refa; Ahmed Arajiga
Azam 0-1 Simba
26/06/2021
Nusu Fainali ASFC
Majimaji, Songea
Refa; Ahmed Arajiga
Yanga 0-1 Simba
25/07/2021
Fainali ASFC
Lake Tanganyika, Kigoma
Refa; Ahmed Arajiga