Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ihefu yaivimbia Yanga

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikieleka ukingoni timu ya Ihefu FC  imeitangazia vita timu ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuchezwa Julai 15 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti Kocha  Mkuu wa kikosi hicho, Zubery Katwila alisema kuwa wamekuja Dar es Salaam kuondoka na pointi sita na sio kushangaa mataa huku nguvu zao zote ni kuelekea kwenye mechi mbili zijazo wakianza na mechi ya kesho dhidi ya Yanga.

"Tunamshukuru Mungu tumefika salama, kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu dhidi ya Yanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ingawa tunajua wazi kuwa tunaenda kucheza na timu bora kwenye ligi ila hilo kwetu halitutishi kwani tuko tayari kupambana mpaka tone la mwisho kwani tumekuja na tahadhari kubwa" alisema Katwila

Aidha Kocha huyo alisema kuwa licha ya ugumu uliopo katika michezo iliyosalia ila watahakikisha wanapambana ili kuhakikisha timu hiyo yenye maskani yake Mbarali jijini Mbeya inasalia kwenye ligi kuu kwa msimu ujao.

"Kila mechi ni ngumu kama unavyojua tuko tayari kupambana katika mechi zetu zote mbili zilizosalia lengo ni kupata pointi sita ambazo zitatuhakikishia kubaki ligi kuu kwa msimu ujao kwani hiyo ndio dhamira yetu kubwa kwa sasa" alisema.

Golikipa mkongwe wa timu hiyo Deogratius Munishi 'Dida' aliyezichezea timu za Simba, Yanga na Azam alisema kuwa licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo ila wamejiandaa vyema kukabiliana na mchezo huo huku akidai kuwa wachezaji wenzake na benchi nzima la ufundi wana ari kuelekea mchezo huo lengo likiwa ni kuipigania timu hiyo inayopigania kuepuka katika janga la kushuka daraja.

"Tunaelekea katika mchezo mgumu ila sisi kama wachezaji na benchi la ufundi chini ya kocha wetu Katilwa tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika michezo yetu iliyosalia ambayo itatupa nafasi kubwa ya kusalia ligi kuu kwa msimu ujao" alisema Dida.

Ihefu iko katika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 35 kwenye msimamo wa Ligi kuu Bara ikiwa imecheza michezo 32 huku ikikabiliwa na wakati mgumu wa kuweza kusalia kwani baada ya kucheza na Yanga kesho itaendelea kusalia kumenyana na timu ya KMC Julai 18.


IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI