Huyu Morrison anavituko nyie!
BAADA ya kuchwa kwa Benard Morrison katika msafara wa wachezaji 25 wa Simba ambao wameelekea Sudan kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh SC, kumeibua kioja na kuanza kuchokozwa huko kwenye mitandao ya kijamii.
Yupo shabiki mmoja aliyeposti na kumuuliza “vipi huko Morrison unapigwa shambulio lingine baada ya lile la awali kulishinda?” Morrison alijibu kwa vikatuni vya kucheka akionyesha kufurahishwa na maneno ya mdau huyo.
Watoto wa mtaani wanasema hana baya na huwa hajali wala nini nyota huyo wa zamani wa Yanga na amekuwa na uamuzi wa papo kwa papo bila kufikiria mara mbilimbili, ndio maana kuna kipindi video yake ilisimbaa akionyesha ishara ya matusi.
Japo sio taarifa za kuziamini lakini inasemekana kwamba Morrison amesusa baada ya kupigwa chini kwani anaonekana alitamani kuwa sehemu ya msafara wa kikosi hicho, lakini kwa mujibu wa maelezo ya kocha wake, Didier Gomes ni kwamba alichagua wachezaji 25 ambao walikuwa tayari zaidi kwa mchezo huo wa ugenini.
Nyota wengine waliopigwa chini kwenye msafara huo ni Junior Lokosa, Ibrahim Ame, na Said Ndemla.