Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata mfanyeje, Niyonzima, Chirwa ndio kiboko yenu

Muktasari:

  • Yanga inahitaji ushindi au sare ya mabao kuanzia 2-2, itafanya mabadiliko ya kimfumo kwa kuwarudisha kikosini viungo Haruna Niyonzima na Deus Kaseke

YANGA tayari imeshatua Zambia tangu jana Alhamisi usiku ambako licha ya kukuta mizengwe iliyoanzishwa na wenyeji Zanaco, kuna sura mpya ambazo zimeshikilia mamilioni yao.

Donald Ngoma na Amissi Tambwe hawajasafiri kutokana na majeruhi, lakini benchi la ufundi lina imani na nguvu mpya kwenye kikosi cha kwanza.

Yanga inahitaji ushindi au sare ya mabao kuanzia 2-2, itafanya mabadiliko ya kimfumo kwa kuwarudisha kikosini viungo Haruna Niyonzima na Deus Kaseke, huku mshambuliaji Obrey Chirwa aliyepangwa pembeni kwenye mechi ya kwanza, akirudishwa  katikati nafasi  ambayo amekuwa akifanya vizuri zaidi pindi anapopangwa.

Faida nyingine kwa Yanga kwa mujibu wa benchi la ufundi ni Zanaco kutowaona Niyonzima na Kaseke katika mechi ya kwanza ambayo hawakupangwa lakini pia kiungo Thaban Kamusoko huenda akarudishwa kucheza namba sita, tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza.

“Tunakwenda ugenini kusaka ushindi na sio vinginevyo. Hatuna hofu yoyote ya kucheza ugenini kwa sababu tuna uzoefu wa kutosha lakini pia ubora wa uwanjani una nafasi kubwa ya kuamua matokeo hivyo tumejipanga kikamilifu na tuna imani kubwa kuibuka na ushindi,” alisema Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi.

Wachezaji Simon Msuva na Niyonzima wamesisitiza kwamba wanaelewa umuhimu wa matokeo na wanachotakiwa kufanya hivyo watafanya kwa vitendo uwanjani na mashabiki wawe na imani nao.

Yanga  imekutana na mtihani wa kwanza kutoka kwa wenyeji wao kwa kubadilishwa uwanja utakaochezwa mechi hiyo kutoka Nkoroma na kuipeleka kwenye uwanja wa taifa wa Zambia uliopo mjini Lusaka.

Ukweli wa taarifa hizo ulithibitishwa na mwandishi wa habari za michezo nchini humo John Banda aliyesema: “Mechi itachezwa kwenye uwanja wa taifa unaoingiza mashabiki 60,000, ambao ndio ulichezewa fainali za Afrika kwa vijana wenye miaka chini ya 20 badala ya ule wa Nkoroma unaoingiza mashabiki 20,000 ambao ndio Zanaco huutumia kwa mechi zake za nyumbani.”

NOTI

Timu yoyote inayofuzu kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huzoa kitita cha  Dola 550,000 (Shilingi 1.2 bilioni) ambazo hutolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Yanga ni wazi kuwa itazitolea macho fedha hizo ambazo zitaiwezesha kuiweka sawa kiuchumi katika kipindi hiki ambacho inakabiliwa na ukata.

Katika mechi tano za mwishoni ambazo Yanga ilicheza ugenini dhidi ya timu za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, timu hiyo imepoteza mechi mbili tu kwa kufungwa bao 1-0 huku wakiibuka na ushindi kwenye mechi tatu. Yanga ikiwa ugenini kwenye mechi hizo tano, imefunga mabao manane na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara nne tu.