Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hat-Trick zaanza kukoleza mzuka

HAT Pict

Muktasari:

  • Wachezaji waliofunga mabao matatu 'Hat-Trick', ni Calvin Kayongo wa Bigman FC katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 3-2, dhidi ya Stand United 'Chama la Wana', mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Oktoba 25, 2026.

HAT-TRICK zimeanza kumiminika katika Ligi ya Championship msimu huu, baada ya kushuhudiwa wachezaji wawili wakifunga, huku ikisubiriwa kuona ikiwa itavunjwa rekodi ya msimu wa 2025-2026, ambao nyota watano tofauti walifunga.

Wachezaji waliofunga mabao matatu 'Hat-Trick', ni Calvin Kayongo wa Bigman FC katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 3-2, dhidi ya Stand United 'Chama la Wana', mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Oktoba 25, 2026.

Mchezaji wa pili ni mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Oscar Paul aliyeifungia katika ushindi wa mabao 5-0, dhidi ya TMA FC ya mjini Iringa, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini, Mbeya, Novemba 1, 2026.

Kwa msimu wa 2025-2026, zilifungwa tano, ambapo waliofunga ni Obrey Chirwa katika ushindi wa Kagera Sugar wa mabao 3-1, dhidi ya Hausung FC, Desemba 2, 2025 na Boniface Mwanjonde wakati Mbeya Kwanza ilipoichapa B19 FC 5-0, Desemba 17, 2025.

Japhet Makarai akaifungia TMA FC ilipoichapa Stand United mabao 4-2, Aprili 19, 2026, akafuatia, Salum Ngadu wa Gunners FC ikiishinda Mbuni FC 3-2, Aprili 20, 2026 na Frank Ikobela wakati Transit Camp ilipoifunga Mbuni 4-3, Juni 14, 2026.