Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hao Yanga mbona mapema tu!

Mbeya. Ni Mapema tu ndivyo unavyoweza kusema mashabiki wa Yanga wameruhusiwa kuingia katika Uwanja wa Sokoine  jijini Mbeya kwa ajili ya kuutazama mchezo dhidi ya Mbeya City saa 10:00.

Mageti ya Uwanja wa Sokoine yalifunguliwa rasmi saa nne kamili ambapo mashabiki wameruhusiwa kuingia huku wengi wakionekana kuwa ni mashabiki wa Yanga tayari kwa kupokea kombe lao.

Hao Yanga mbona mapema tu!

Akizungumza na Mwanaspoti mmoja wa mashabiki wa Yanga Ellen Mathias anasema baada ya muda mrefu hatimaye kiu yao ya makombe imeisha rasmi na sasa ni mabingwa

“Nashukuru GSM kupitia injinia Hersi wametufuta machozi kwa sasa tunafuraha sana haielezeki na pia ukame wa makombe sasa basi tumechukua kila kitu kwani julai 2 tunamfunga Coastal mapema tu “. amesema Ellen.

Ndani ya Uwanja mashabiki wanaonekana wakiwa wamekaa  kwa utulivu huku wengine wakicheza muziki unaopigwa ndani ya Uwanja na jukwaa rasmi la kukabidhi Ubingwa limeshakamilika.