Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hababuu aanza na Rayon Sports

HABABUU Pict
HABABUU Pict

Muktasari:

  • KVZ iliondoka Zanzibar Julai 20, 2026 kwenda Rwanda kushiriki michuano hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza ambapo Jumapili hii, itaikabili Rayon Sports.

KOCHA Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ, Hababuu Ali amesema kikosi chake kimefika salama nchini Rwanda na kinaedelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Kagame dhidi ya Rayon Sports.

KVZ iliondoka Zanzibar Julai 20, 2026 kwenda Rwanda kushiriki michuano hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza ambapo Jumapili hii, itaikabili Rayon Sports.

Hababuu amesema KVZ ina malengo mawili katika michuano hiyo ikiwemo kujenga uzoefu wa kimataifa na maandalizi kwa ajili ya kushiriki Ligi ya Mabingwa  Afrika.

Amesema mashindano hayo ni fursa muhimu kwa wachezaji wake kupata uzoefu wa kucheza mechi za kimataifa na timu zenye ushindani mkubwa jambo litakalosaidia kuimarisha kikosi hicho.

HABA 01

“Tumejipanga kucheza na Rayon, tumefika salama na tunafanya mazoezi, hivyo tunaamini tutafanya vizuri katika mchezo huu,” amesema.

Amesema, licha ya timu hiyo kupangwa katika kundi C lenye mabingwa na wazoefu wa michuano hiyo, lakini sio sababu ya kushindwa kutimiza malengo na itakuwa kipimo kizuri kwao.

Amesema kwa kipindi hiki kupata mechi za ushindani wa kiwango cha kimataifa si jambo rahisi, hivyo wanahakikisha wanaitumia fursa hiyo kujipima dhidi ya timu zenye ubora.

HABA 02

Alibainisha, benchi la ufundi limejipanga kuhakikisha timu inatoa ushindani katika kila mchezo, huku lengo likiwa si tu kupata matokeo mazuri bali kujenga kikosi imara kitakachokuwa tayari kwa changamoto za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika Kundi C, KVZ baada ya kumalizana na Rayon ya Rwanda, Julai 29 itaikabili Al Hilal ya Sudan, kisha itamaliza makundi Agosti 1 kupambana na Tusker ya Kenya.