Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola mikono juu kwa Madrid

Muktasari:

  • KATIKA toleo lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, tuliona jinsi Mwandishi Marti Perarnau alivyaoanza mahojiano na Kocha Pep Guardiola kubwa ikiwa ni kuhusu tathmini yake ya mwaka mzima aliokuwa na timu ya Bayern yaani msimu wa 2013/14 ambao ulikuwa umefikia ukingoni. Sasa endelea…

KATIKA toleo lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, tuliona jinsi Mwandishi Marti Perarnau alivyaoanza mahojiano na Kocha Pep Guardiola kubwa ikiwa ni kuhusu tathmini yake ya mwaka mzima aliokuwa na timu ya Bayern yaani msimu wa 2013/14 ambao ulikuwa umefikia ukingoni. Sasa endelea…

“Kwa hali hiyo katika mazingira kama hayo mwaka umekuwa wa mafanikio, mataji manne kati ya sita, tumepoteza kwenye Ligi ya Mabingwa lakini jinsi tulivyopoteza ndilo jambo lililotuachia hasira na si kwamba tumefikia hadi hatua ya nusu fainali ambayo ina maana kubwa.

“Hakuna namna yoyote ya kujitetea kwa namna tulivyopoteza mechi ya Ligi ya Mabingwa kwa Real Madrid, nahitaji kuinua mkono na kukubali kushindwa lakini kimsingi nilifanya vizuri. Nimekuja katika nchi mpya kuiongoza timu iliyotoka kushinda mataji matatu nikiwa na wachezaji wawili tu wapya na zaidi ya hilo nimekuja katika lugha mpya.

“Na hilo la lugha nalo ni changamoto kwa sababu pia unahitaji kujieleza vizuri lakini lingine ni kuijua vizuri kiasi cha kutosha kwa sababu unawasiliana na wachezaji ambao wanatakiwa wapate vizuri kile unachowaambia.

“Katika hilo la lugha pia ni lazima uwe na msamiati mzuri na sahihi na misamiati yangu bado haijawa ya kiwango kizuri, unaweza kutafakari mwaka mmoja uliopita nikisikia watu wanasalimiana sijui salamu hiyo inamaanisha nini, mchana au asubuhi lakini si rahisi kuwa na misamiati mizuri ya kukufanya uwe na uhakika wa kufikisha ujumbe kwa wachezaji.

Perarnau: Kumrithi Heynckes (Jupp) kunatajwa kuwa ni changamoto kubwa, unasemaje kuhusu hilo?

Pep: Ndio, lakini pia hata ushindi wetu mwingi ulitokana na kazi iliyofanywa na Jupp mwaka jana pamoja na hulka ya ushindani iliyokuwa kwenye timu, wachezaji walijiona wao ni washindi na ndio maana ikawa muhimu kubeba taji la ligi na lile la Ujerumani.

“Mataji hayo yaliongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji, walijiona wana uwezo wa kushinda baada ya kuwa tayari wameshinda kila kitu, kama tungepoteza taji la Ujerumani miezi ambayo ingefuata pengine ingekuwa migumu mno kwetu

“Nilikuwa Kocha Barcelona pia, mara tu baada ya kushinda mataji matatu lakini walifanya hivyo mimi nikiwa kwenye benchi na hapa nimechukua nafasi ya Jupp, hakika hiyo ni changamoto lakini nilitaka kujipima kwa kuja nchi tofauti ambako ningejifunza lugha mpya na kuwa kocha katika timu yenye mafanikio ya kipekee.

“Nilijua hili lingekuwa jambo gumu, nimeshinda mataji manne msimu huu, lakini kwangu hilo si jambo muhimu sana, jambo muhimu ni kutengeneza kitu ambacho kitakuwa mimi ndiye mwenyewe na hapa namaanisha staili ya uchezaji kwenye timu.

Perarnau: Je, ni kweli kila unachokifanya kutoka Barcelona kinakuwa ni mgongano wa kiutamaduni?

Pep: Hiyo ni kweli kwa sababu, mimi ni shabiki mkubwa wa uchezaji wa kuzingatia maeneo, kujazana na kufanya vurugu katika eneo la penalti la timu pinzani na kutowapa nafasi ya kuondoka eneo hilo, ni timu chache mno zinazocheza hivyo. Barca wanafanya hivyo kama anavyofanya Paco Jemez (kocha wa Rayo Vallecano kabla ya kuihama timu hiyo) lakini kimsingi ni kama hakuna timu inayofanya hivyo.

“Timu nyingi zinapenda kusubiri nafasi ya kufanya mashambulizi ya kushitukiza. Pia, kushambulia kwa kuzingatia maeneo, nalo ni jambo gumu kwa sababu wachezaji wako wanahitaji uvumilivu kwa kiasi kikubwa, ina maana kuna mchezaji binafsi ambaye analazimika kutambua anaweza asiwe katikati ya tukio kwa muda fulani lakini bado anaisaidia timu kwa hicho anachokifanya.

“Lakini pia pale anapoingilia katika kuwania mpira yeye tu anaweza kuwa na mchango mkubwa, ili kufanikisha hilo mchezaji anatakiwa awe mwenye kujijengea dhana ya uvumilivu, awe mwenye kujitoa, ni lazima ukubali si wakati wote utakuwa katikati ya tukio uwanjani na kazi yako itakuwa kufungua vyumba au kutanua uwanja kwa wachezaji wenzako.

Itaendelea Jumamosi