Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gomes v Nabi kazi ipo!

Muktasari:

MABOSI wa Yanga wajanja sana, wamechungulia namna mambo yao yalivyo kulinganisha na watani wao, Simba na fasta wakajiongeza wakiamua kubadili gia hewani kwa kushusha kocha mpya.

MABOSI wa Yanga wajanja sana, wamechungulia namna mambo yao yalivyo kulinganisha na watani wao, Simba na fasta wakajiongeza wakiamua kubadili gia hewani kwa kushusha kocha mpya.

Yanga imemleta Kocha Nasreddine Nabi, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Tunisia ili awe bosi wa benchi lao la ufundi akichukua nafasi ya Cedric Kaze, ikiwa ni baada ya kuachana na Mfaransa Sebastian Migne waliyekuwa wameshakubaliana naye kila kitu na kutofautiana mambo madogo tu.

Nabi hakuwa na timu tangu alipotimuliwa na Al Merrikh ya Sudan aliyoiongoza katika mechi tatu tu za Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwamo dhidi ya Simba iliyoisha kwa suluhu mjini Khartoum Machi 6 mwaka huu.

Ujio wa kocha huyo unaonekana unaweza kuwa ukombozi kwa Yanga ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa na kiti cha moto kwa makocha kutokana na wengi wao kuifundisha kwa muda mfupi na kujikuta wakitimuliwa.

Lakini kwa upande mwingine, Nabi anaonekana anaweza kuwa mshindani halisi wa kocha wa Simba, Didier Gomes ambaye tangu amefika hapa nchini kuinoa timu hiyo imekuwa moto wa kuotea mbali katika mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tathmini iliyofanywa na Mwanaspoti imebaini kwamba ujio wa Nabi unaweza kuleta ushindani mkali baina yake na Gomes kutokana na wasifu wao na mafanikio waliyowahi kuyapata kabla hawajaja nchini kwa nyakati tofauti na hasa uzoefu wao katika soka la Afrika kwa ngazi ya klabu.


WASOMI

Gomes na Nabi wote sio makocha wa kubabaisha, wamesota darasani hasa na ni wamiliki wa leseni ya juu ya ukocha inayotolewa na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA ProLicence). Gomes aliipata leseni yake Ufaransa, Nabi yeye aliipata Ubelgiji.


MATAJI

Nabi tayari ameshatwaa taji moja ambalo ni Kombe la Shirikisho akifanya hivyo mwaka 2012 alipokuwa akiinoa AC Leopards ya Congo na kiujumla tangu alipoanza ukocha ameshinda mataji 6.

Mbali ya taji la Kombe la Shirikisho, Nabi ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu ambayo moja ni la Ligi ya Congo Brazzavile alilotwaa msimu wa 2016/2017 akiwa na AC Leopards, pia Ligi Kuu ya Sudan akiwa na Al Hilal Omdurman 2014/2015 na ubingwa wa Ligi Kuu ya DR Congo akiwa na DC Motema Pembe msimu wa 2004/2005.

Amechukua pia Kombe la Congo akiwa na AC Leopards msimu wa 2016/2017 na pia amewahi kutwaa taji la mashindano ya U-16 Youth League msimu wa 2003/2004 akiwa na timu ya vijana ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Kwa upande wa Gomes, yeye ametwaa jumla ya sita katika maisha yake ya ukocha kama Nabi ambaye watakutana kwa mara ya kwanza katika mechi ya marudiano ya Kariakoo Derby, Mei 8 jijini Dar.

Mfaransa huyo aliyekuwa Al Merrikh kabla ya kutua Simba mapema mwaka huu, ametwaa kombe la Cameroon na pia mataji mawili ya Elite One mara mbili ambazo ni 2014 na 2015 huku pia akitwaa Kombe la Addis Ababa City mwaka 2018

Ametwaa taji la Ligi Kuu ya Guinea, msimu wa 2018/2019 ambao pia walitwaa Kombe la Guinea.


WABABE AFRIKA

Hapa Gomes amezidiwa kete kwani mwenzake Nabi amewahi kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na AC Leopards ya Congo mwaka 2012.

Lakini hajaishia hapo tu kwani amewahi kuiongoza Al Hilal kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2015 na amewahi kuiongoza DC Motema Pembe kuingia hatua hiyo katika Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2011.

Kwa upande wa Gomes, mafanikio makubwa kwake katika mashindano ya klabu Afrika yalikuwa ni kuiongoza Coton Sports ya Cameroon kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2014.

Pia msimu wa 2019/2020 aliifikisha Ismaily ya Misri katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Uarabuni na msimu huu kaiongoza Simba kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


UZOEFU MKUBWA

Kitendo cha kufundisha idadi kubwa ya timu barani Afrika kimewafanya Nabi na Gomes kuwa na uzoefu wa kutosha wa soka la Afrika.

Kocha Nabi amefundisha kwa muda wa zaidi ya miaka 16 barani Afrika katika timu sita kati ya nane alizowahi kufundisha katika maisha ya soka. Klabu hizo za Afrika ni AC Leopards, DC Motema Pembe, Al Hilal Omdurman, Ismaily, Al Merrikh na Al Ahli Benghazi ya Libya, wakati Gomes yeye amefundisha soka Afrika kwa muda wa miaka nane na katika kipindi chote hicho timu tisa zimefaidi huduma yake. Amefundisha timu 12.

Gomes amefundisha Rayon Sports, Coton Sports, CS Constantine, JSM Skikda, Ethiopian Cofee, Horoya, Ismail Mustafa, Al Merrikh.