Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold FC yapata basi jipya

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imemaliza tatizo la usafiri kwa timu ya Geita Gold FC, baada ya kuwanunulia basi jipya.

Basi hilo limewasili jana Alhamisi mjini Geita baada GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kumega sehemu ya udhamini huo kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri kwa timu hiyo.

Meneja Mwandamizi anayeshughulikia maendeleo ya jamii, Gilbert Mworia amesema kukabidhiwa kwa basi hilo ni itakuwa chachu ya ushindi wa timu hiyo kuelekea mchezo kati yake na Yanga kesho Jumamosi.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanka wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Amesema GGML imetoa basi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa uwajibikaji kwa jamii - CSR.

Mworia amesema basi hilo linatarajiwa kukabidhiwa kwa uongozi wa timu katika hafla itakayofanyika wiki ijayo.

“Basi hili litasaidia maendeleo ya timu yetu katika safari zake pindi wanaposhiriki michezo ya ligi kuu kuzunguka mikoa mbalimbali na hata nje ya nchi pale itakapolazimika,” amesema.

Amesema ufadhili mwingine ni wa masuala ya vifaa vya michezo ikiwamo jezi, bukta, viatu na vifaa vingine.

Amesema katika ujenzi wa uwanja huo ambao ulisimama kwa muda, GGML imejipanga kuendeleza ujenzi kwa nguvu zote ili timu ipate mazingira mazuri ya michezo.

Ameahidi kampuni hiyo ya madini itaendelea kufadhili timu hiyo na hata kushiriki katika michezo ya ndani na nje ili kuchochea maendeleo ya michezo nchini hasa ikizingatiwa michezo ni ajira.