Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chipukizi hali tete Ligi Kuu Zanzibar

CHIPUKIZI Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo imeruhusu mabao matano ikichangiwa na kipigo cha 4-1 dhidi ya Uhamiaji. Pia imefungwa 1-0 na JKU, huku sare ya kwanza kwa Black Sailors timu hizo zikitoka 0-0 ikiwa ni matokeo mazuri pekee iliyopata hadi sasa.

TIMU ya Chipukizi, imeanza msimu wa 2026-2027 katika Ligi Kuu Zanzibar vibaya baada ya kuambulia vipigo viwili na sare moja.


Timu hiyo imeruhusu mabao matano ikichangiwa na kipigo cha 4-1 dhidi ya Uhamiaji. Pia imefungwa 1-0 na JKU, huku sare ya kwanza kwa Black Sailors timu hizo zikitoka 0-0 ikiwa ni matokeo mazuri pekee iliyopata hadi sasa.

Katika mchezo uliochezwa Septemba 6, 2026 dhidi ya JKU, Chipukizi imeonekana kuwa na mabadiliko ya uchezaji, lakini kikosi hicho kilishindwa kuhimili mashambulizi ya wapinzani wao na kujikuta kikiruhusu bao dakika ya 83 lililofungwa na Tarik Mkonga.

Kocha Mkuu wa Chipukizi, Suleiman Mohamed ‘Mani Gamera’ amesema mchezo huo haukuwa mbaya kwa pande zote mbili kwani mpango ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Amesema, wapinzani wao JKU msimu uliopita walikuwa katika mbio za ubingwa na wana wachezaji wazoefu, ndiyo sababu ya kikosi chake kupoteza.

“Chipukizi haikufanya vizuri msimu uliopita, hivyo ilijiandaa kwa kusajili zaidi na muunganiko wa timu haujawa mzuri lakini nawapongeza wachezaji kwa kupambana,” amesema.

Alieleza kuwa, wachezaji wa kikosi hicho wamecheza kwa maelekezo na hawakutoka nje ya mfumo na anachofurahishwa ni kuonesha kitu kizuri kwenye mchezo huo.

Alifafanua kwamba, kwa sasa mabadiliko yanayoonekana kwenye kikosi hicho, Chipukizi haiwezi tena kuruhusu mabao mengi kama ilivyotokea katika mechi dhidi ya Uhamiaji.

Chipukizi sasa inajiandaa na mchezo wa nne kesho Jumatano dhidi ya Kipanga kwenye Uwanja wa Mao B uliopo Unguja, ikikamilisha mechi nne ugenini kabla ya kurudi kisiwani Pemba.