Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamera apewa miwili Chipukizi

GAMERA Pict

Muktasari:

  • Mani Gamera msimu uliopita alikuwa anaifundisha timu ya Fufuni iliyopanda daraja na kuwa tishio Ligi Kuu Zanzibar, kabla ya kumalizika msimu aliamua kuachana nayo.

TIMU ya Chipukizi imemtambulisha rasmi Suleiman Mohamed ‘Mani Gamera’ kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Mani Gamera msimu uliopita alikuwa anaifundisha timu ya Fufuni iliyopanda daraja na kuwa tishio Ligi Kuu Zanzibar, kabla ya kumalizika msimu aliamua kuachana nayo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Chipukizi United, Kheri Kidema, amesema timu hiyo imemchagua kocha huyo kutokana na uwezo wake wa soka Zanzibar.

Kidema amesema kocha huyo ameshaanza kazi mara tu alipotambulishwa na msimu huu malengo yao yatakuwa makubwa ikilinganishwa na msimu uliopita.

Amesema sababu ya kufanya maboresho hayo ni kurudisha heshimu ya Chipukizi United ambayo ilikuwa imepotea kwa miaka ya hivi karibuni.

“Kocha amesaini mkataba wa miaka miwili, naamini uwepo wake utarejesha furaha iliyokuwa imepotea kwa misimu miwili mfululizo,” amesema.

Kidema amesema sasa hivi ratiba nyingine zitaendelea kama kutambulisha wachezaji wapya, huku mazoezi yakianza licha ya kwamba wachezaji wote bado hawajaripoti.