Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu ya Chipukizi yambeba Gamera

KILIO

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya Chipukizi zinasema kwamba, timu hiyo imefyeka benchi zima la ufundi, hivyo Gamera anakwenda kulisuka upya kwa ajili ya kupambana kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Zanzibar.

BAADA ya timu Wembe kutia nia ya kumtaka aliyekuwa Kocha Mkuu wa Fufuni, Suleiman Mohamed ‘Mani Gamera’, sasa upepo umegeuka na kocha huyo msimu ujao atainoa Chipukizi iliyopo kisiwani Pemba.

Taarifa kutoka ndani ya Chipukizi zinasema kwamba, timu hiyo imefyeka benchi zima la ufundi, hivyo Gamera anakwenda kulisuka upya kwa ajili ya kupambana kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Zanzibar.

Mwanaspoti limezungumza na Gamera ambaye amekiri kumwaga wino katika timu hiyo iliyopo Pemba licha ya misukosuko aliyokutana nayo msimu wa 2025-2026 wakati akiinoa Fufuni ya kisiwani humo.

“Ni kweli nimeshajiunga na Chipukizi, mashabiki na wadau wa soka wasubirie mazuri kutoka kwangu msimu ujao,” amesemaGamera.

Alipoulizwa kuhusu awali kutakiwa na Wembe, Gamera amesemakweli timu hiyo ilikuwa inamuhitaji lakini walishindwa kuelewana na kwasasa wamechelewa kwani hawakuweza kucheza kete zao zao vizuri.

Gamera amesemaanatambua kuwa anaipokea Chipukizi katika kipindi kigumu ila anaamini kwa uwezo alionao atairejeshea heshima yake ya awali.

Kocha huyo baada ya kuachana na Fufuni, timu ya KVZ, Wembe na Mafunzo zilitupa karata zao kuwania saini yake, lakini Chipukizi ikafanikiwa kumnasa.

Wakati huohuo, chanzo cha ndani ya timu ya Wembe iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu Zanzibar msimu ujao wa 2026-2027, kimeliambia Mwanaspoti kwamba wameshangazwa na taarifa za Gamera kusaini Chipukizi kwani viongozi walikuwa katika majadiliano ya kumsaini.

“Tulikuwa na mazungumzo ndani ya timu yetu kwa ajili ya kumsaini Gamera lakini nimeshangazwa na taarifa za kujiunga na Chipukizi, bado tunaumiza vichwa,” kilisema chanzo hicho.