Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Filbert Bayi kukomaa na ukuzaji wa vipaji vya michezo

RIADHA Pict

Muktasari:

  • Amewataka wahitimu hao kuendelea kujiamini katika safari yao ya elimu, kuheshimu wazazi na walimu, pamoja na kuweka kipaumbele katika masomo na michezo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi na Shule za Filbert Bayi, Filbert Bayi amesema bodi itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo, madarasa na walimu wenye mafunzo bora ili kuimarisha elimu na kukuza vipaji vya wanafunzi.

Amesema dhamira ya taasisi hiyo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora inayojenga umahiri wa kitaaluma na maadili mema, kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.

“Tutaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia, kuwekeza katika madarasa bora, viwanja bora vya michezo na walimu waliofunzwa vyema,” amesema Bayi.

Amesema taasisi hiyo haijajikita katika kutoa elimu ya darasani pekee, bali pia inataka kujenga familia ya wanafunzi wenye nidhamu, upendo na misingi imara ya maisha.

Akizungumzia mchango wa walimu, Bayi amesema kazi ya kuwafundisha watoto wadogo inahitaji uvumilivu na upendo, akiwapongeza walimu wa elimu ya awali kwa kuwalea na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Shule za Filbert Bayi, Elizabeth Mjema, alisema wanafunzi hao wamekuwa wakishiriki michezo mbalimbali kupitia matamasha ya michezo na vipindi vya kawaida vya kukuza vipaji katika kampasi za Kimara na Kibaha.

Amesema shule hizo zinaona michezo kuwa sehemu muhimu ya malezi na maendeleo ya wanafunzi, ikizingatiwa kuwa inasaidia kujenga afya na nidhamu.

“Elimu ni ufunguo wa maisha, lakini michezo ni afya na nidhamu,” amesema.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya shule hizo, mkurugenzi huyo amesema zaidi ya asilimia 95 ya wanafunzi wa elimu ya awali wameweza kumudu stadi mbalimbali za msingi, zikiwamo kutambua herufi, namba, rangi na lugha za Kiingereza na Kiswahili kwa kiwango cha kuridhisha.

Aidha, amewataka wazazi kuendelea kushirikiana na walimu katika kuwalea watoto wao, akiwashauri kutenga angalau dakika 15 kila siku kuwasaidia kujifunza wanapokuwa nyumbani, kupunguza muda wa kutumia simu na televisheni, na kuongeza muda wa kucheza na kujifunza pamoja.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau amesema kuna umuhimu wa kuwajengea watoto misingi ya nidhamu, kujiamini na kutumia teknolojia vizuri ili kuwaandaa kukabiliana na changamoto za maisha, akitaja michezo kuwa miongoni mwa maeneo yanayopaswa kupewa nafasi katika ukuaji wao.

Tandau ameyasema hayo wakati akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali (Pre-Unit) wa Shule za Filbert Bayi, yaliyofanyika katika kampasi ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Amesema watoto wanapohitimu elimu ya awali na kujiandaa kuingia darasa la kwanza, wanahitaji kuendelea kujengewa misingi itakayowasaidia kufikia malengo yao, ikiwamo nidhamu, heshima na matumizi sahihi ya teknolojia.

Amewataka wahitimu hao kuendelea kujiamini katika safari yao ya elimu, kuheshimu wazazi na walimu, pamoja na kuweka kipaumbele katika masomo na michezo.