Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fikiri aandaa silaha za kuichapa Pamba Jiji

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Pamba ambayo ipo kwenye mstari mwekundu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, imefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu kati ya 11 iliyocheza na kupata sare tatu hivyo imekusanya pointi sita kati ya 33 ambazo ilitakiwa kuwa nayo ikijiweka kwenye wakati mgumu wa kubaki kwenye ligi kuu kwa msimu ujao.

COASTAL Union inakwenda kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji ikiwa na kazi ya kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita, lakini safari hiyo haitakuwa nyepesi kutokana na wenyeji wake kuwa na presha kubwa ya kutafuta ushindi ili kujinasua kwenye eneo gumu la msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Pamba ambayo ipo kwenye mstari mwekundu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, imefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu kati ya 11 iliyocheza na kupata sare tatu hivyo imekusanya pointi sita kati ya 33 ambazo ilitakiwa kuwa nayo ikijiweka kwenye wakati mgumu wa kubaki kwenye ligi kuu kwa msimu ujao

Kwa upande wa Coastal, nayo haipo kwenye wakati mzuri ikiwa na pointi 14 kwenye michezo 11 ambayo imecheza hado sasa ikiwa inashika nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi, tofauti ni pointi 16 dhidi ya vinara wa ligi Simba.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, kocha wa Coastal, Fikiri Elias, amesema wanawafuata wapinzani wao kwa tahadhari kubwa kwa kutambua kwamba Pamba itakuwa na msukumo mkubwa wa kutafuta ushindi.

“Tunajua tunakwenda kucheza na timu ambayo inahitaji pointi kwa hali yoyote ile. Pamba itakuwa na hesabu zake za kutafuta ushindi kwa sababu inahitaji kutoka kwenye eneo ililopo kwenye msimamo, hivyo hatuwezi kwenda tukiwa tumepuuza mchezo huo,” amesema Fikiri.

Kocha huyo amesema katika maandalizi yao wameweka mkazo mkubwa kwenye eneo la ulinzi ambalo limekuwa likiwapa shida kutokana na kuruhusu mabao mengi ambayo hayakuwa sehemu ya malengo yao.

“Tumekuwa tukifanya kazi kubwa kwenye eneo la beki kwa sababu tumekuwa tukiruhusu mabao mengi ambayo hayakuwa kwenye malengo yetu. Tunataka kurekebisha makosa hayo ili timu iwe imara zaidi tunapokuwa hatuna mpira,” amesema.

Ameongeza mbali na ulinzi, wamefanyia kazi pia muunganiko wa wachezaji na safu ya ushambuliaji ili kuongeza uwezo wa kutengeneza nafasi na kuzitumia kuwa mabao.

“Tumeboresha pia muunganiko wa timu na eneo la ushambuliaji. Tunataka wachezaji waelewane vizuri zaidi, tutengeneze nafasi nyingi na tuwe na nguvu ya kuzitumia nafasi hizo kupata mabao,” amesema kocha huyo.