Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lawi avunja ukimya Azam FC

LAWI Pict

Muktasari:

  • BEKI wa kati wa Azam FC, Lameck Lawi ameibuka na kuvunja ukimya akifuta uvumi wa taarifa za kuomba kuondoka katika timu hiyo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

BEKI wa kati wa Azam FC, Lameck Lawi ameibuka na kuvunja ukimya akifuta uvumi wa taarifa za kuomba kuondoka katika timu hiyo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Lawi amesema taarifa zinazoendelea kuzungumzwa kuhusu yeye kuomba kuondoka ndani ya timu hiyo sio za kweli, isipokuwa kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara ni changamoto kwake ya kuzidi kuimarisha kiwango.

“Mchezaji mzuri ni yule anayekubali changamoto na kutafuta namna nzuri ya kuzitatua, ni kweli nimekuwa katika kipindi kigumu cha kutocheza mara kwa mara, ila inanipa fursa ya kupambana zaidi ili kushawishi benchi la ufundi,” amesema Lawi.

Beki huyo aliyejiunga na Azam FC, Julai 3, 2025, akitokea Coastal Union ya Tanga, amesema ushindani katika timu hiyo ni jambo analofurahia kwa sababu anazidi kujifunza kwa nyota wenzake wenye uzoefu, ili awe bora zaidi.

“Nafurahia sehemu niliyopo na malengo yangu ni kuendelea kufanya vizuri kila nitakapopewa nafasi ya kuonyesha kipaji changu uwanjani, tuko wachezaji wazuri katika kila eneo, jambo ambalo linaongeza ushindani kwa kila mmoja wetu pia.”

Nyota huyo aliyegeuka lulu sokoni baada ya vigogo wa Simba na Yanga kuiwinda saini yake kabla ya Azam FC kumnasa Julai 3, 2025, alisaini mkataba wa miaka miwili hadi Juni 30, 2027, ukiwa na kipengele cha kuongeza mmoja.

Licha ya msimu wa 2025-2026, kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge, lakini msimu huu wa 2026-2027, umekuwa mgumu zaidi kwa beki huyo kutokana na maingizo mapya kikosini.