Fernandes aifuata Manchester United
Muktasari:
Fernandes aliweka picha katika mtandao alipohojiwa kuhusu mpango wake wa kutua Man United ambapo alithibitisha kuwa alikuwa njiani kwenda Manchester.
London, England. Nahodha wa Sporting Lisbon ya Ureno, Bruno Fernandes ametua Manchester United kwa vipimo vya afya.
Fernandes ameonyesha furaha baada ya mpango wa kujiunga na Man United kukamilika.
Kiungo huyo anatarajiwa kutia saini mkataba baada ya upimaji wa afya kukamilika. Awali, kulikuwa na mvutano baina ya klabu hizo kuhusu kiwango cha fedha.
Fernandes aliweka picha katika mtandao alipohojiwa kuhusu mpango wake wa kutua Man United ambapo alithibitisha kuwa alikuwa njiani kwenda Manchester.
Alipoulizwa na mwandishi wa habari kama anajiandaa kwenda kucheza Ligi Kuu England, Fernandes alijibu kuwa siku zote ilikuwa hivyo.
Lakini alipoulizwa kama kuhusu uhamisho wake, alisema kila kitu kinakwenda sawa. Fernandes alitarajiwa kwenda Manchester leo kupima afya.