Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto arejea kwa kishindo Azam FC

FEI Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo ambaye alionekana kupata maumivu katika mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Oktoba 31, 2026, ameliambia Mwanaspoti kwamba mapumziko aliyopatiwa yamemsaidia kurejesha nguvu na kuondoa uchovu uliokuwa ukimkabili, huku akieleza kuwa tayari ameanza kufanya mazoezi binafsi na anatarajia kuungana na wenzake kwenye mazoezi kamili wakati wowote.

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ametangaza kurejea katika hali nzuri kiafya baada ya mwili wake kukumbwa na uchovu mkubwa uliomlazimu kupumzika, akisema yuko tayari kurejea kwenye majukumu ya kikosi hicho.

Kiungo huyo ambaye alionekana kupata maumivu katika mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Oktoba 31, 2026, ameliambia Mwanaspoti kwamba mapumziko aliyopatiwa yamemsaidia kurejesha nguvu na kuondoa uchovu uliokuwa ukimkabili, huku akieleza kuwa tayari ameanza kufanya mazoezi binafsi na anatarajia kuungana na wenzake kwenye mazoezi kamili wakati wowote.

“Afya yangu imeimarika, nilikuwa nimechoka sana lakini baada ya kupata mapumziko nimeanza kujisikia vizuri. Nimeanza mazoezi binafsi na wakati wowote kuanzia kesho nitaungana na wenzangu kwenye mazoezi ya timu,” amesema.

Hatua hiyo ni habari njema kwa kocha Florent Ibenge ambaye anahitaji huduma ya kiungo huyo katika kipindi ambacho Azam inaendelea kupambana kwenye Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi.

Ibenge aliwahi kuzungumzia kuhusu kumlinda mchezaji huyo akisema: “Natamani afunge mabao mengi zaidi na ikiwezekana achukue kiatu kwani hilo litampa thamani kubwa, lakini timu pia inamtegemea ndiyo maana nampa nafasi zaidi ya kupumzika.”