Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome, Chama kwenye vita ya tuzo

TUZO Pict

Muktasari:

  • Sherehe hizo za utoaji tuzo zilizopangwa kufanyika Desemba 12, 2026 jijini Arusha, zimewakutanisha mafundi hawa wawili kwenye vipengele vya Kiungo Bora na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC, jambo linaloashiria ushindani mkali wa ubunifu, mbinu na uwezo wao uwanja.

KIUNGO wa Yanga, Pacome Zouzoua na wa Simba, Clatous Chama, wameingia kwenye vita ya kuwania tuzo mbili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) msimu wa 2025-2026.

Sherehe hizo za utoaji tuzo zilizopangwa kufanyika Desemba 12, 2026 jijini Arusha, zimewakutanisha mafundi hawa wawili kwenye vipengele vya Kiungo Bora na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC, jambo linaloashiria ushindani mkali wa ubunifu, mbinu na uwezo wao uwanja.

Pacome Zouzoua amekuwa na msimu wa kipekee sana ndani ya kikosi cha Yanga 2025-2026 ambako alicheza mechi 22 akifunga mabao tisa na asisti nne kabla ya kupata majeraha Juni 30, 2026, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam ambako Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kwa upande wake, Clatous Chama ambaye msimu uliopita alikuwa na kiwango bora akirejea Simba dirisha dogo alipotokea Singida Black Stars, kiungo huyo kwenye mechi 23 alifunga mabao sita na kutoa asisti nne.

CHAM 03

Mbali na Pacome na Chama, nyota wengine wanaowania tuzo ya kiungo bora ni Allan Okello ambaye msimu uliopita aliitumikia Yanga na sasa anakipiga AS FAR Rabat ya Morocco. Kiungo huyo Mganda kwenye mechi 24 alifunga mabao 14 na asisti nane.

Mwingine ni Feisal Salum 'Fei Toto' wa Azam FC, Max Nzengeli wa Yanga. Kwa upande wa mchezaji bora ukiwatoa viungo hao wapo pia mabeki Ibrahim Bacca wa Yanga na Rushine De Reuck wa Simba na mshambuliaji Mossi Nduwumwe aliyekuwa Singida Black Stars ambaye pia ametajwa katika kipengele cha Mfungaji Bora.

Tuzo zingine zinazoweza kuwa na mvuto ni kwa wanaowania Kocha Bora ambapo kuna Florent Ibege wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije wa TRA Unired na Steve Barker wa Simba SC.

Kipa Bora wanaowania ni Djigui Diarra wa Yanga, Aishi Manula (Azam FC), Djibrilla Kassali (Simba), huku upande wa Beki Bora kuna Bacca, Rushine na Ibrahim Imoro wa Singida Black Stars. Pia Tuzo ya Mfungaji Bora, ametajwa Nduwumwe.

Azam FC midfielder Feisal “Fei Toto” Salum. PHOTO | COURTESY

Tuzo ya Mchezaji Bora chipukizi wanaowania ni Abdulkarim Kiswanya (Namungo), Ashrafu Kibeki (Azam FC) na Juma Abushiri (Fountain Gate). Mwamuzi Bora kuna Ahmed Arajiga, Katanga Hussein na Sifu Amon. Timu yenye nidhamu, Fountain Gate, KMC FC na Mbeya City.

Mchezaji Bora Kombe la Shirikisho la Azam, Anicet Oura (Simba), Chama wa Simba na Idd Nado wa Azam FC. Kipa Bora Kassali, Metacha Mnata (Singida) na Zuberi Foba wa Azam huku Tuzo ya Mfungaji Bora ikienda kwa John Chinguku (Magnet FC).

Kwa upande wa soka la wanawake wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora ni Aisha Mnunka (Simba), Ester Maseke (JKT Queens), Jamila Rajabu (JKT Queens), Jentrix Shikangwa (Simba Queens) na Jeaninne Mukandayisenga (Yanga Princess).

Kipa Bora wanaowania ni Gelwa Yona (Mashujaa Queens), Rita Akarekor (Yanga Princess) na Ruth Aturo (Simba Queens). Kwa upande wa mfungaji bora ni Jeannine Mukandayisenga (Yanga Princess).

Kocha Bora wanaowania ni Edna Lema (Yanga Princess), Kessy Abdallah (JKT Queens) na Mussa Hassan 'Mgosi' (Simba Queens). Mchezaji Bora Chipukizi kuna Bahati Kizanguzi (Bunda Queens), Elizabeth Mwiti (Simba Queens) na Jamila Athumani wa Tausi FC.

RUSH 03

Timu yenye nidhamu Alliance Girls, Ceasiaa Queens na Simba Queens, mwamuzi bora Anitha Kisoma, Monica Wazael na Tatu Malogo

Tuzo zingine ni Mwamuzi Msaidizi Bora kuna Maria Mwakitalima, Sikudhani Mkurungwa na Zawadi Yusuph.

Wanaowania Mchezaji Bora NBC Championship ni Denis Mushi (Polisi Tanzania), Maulid Juma (Geita FC), Obrey Chirwa (Kagera Sugar).

Tuzo ya Mchezaji Bora First League kuna Ally Mwinjuma (NKIM FC), Danford Kaswa (Bandari Tanzania) na George Komba (Rhino Rangers).

Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu ya NBC U-20 yupo Abdallah Mkude (Azam FC), Mahsen Saleh (Yanga) na Said Nkondo (JKT Tanzania).

Tuzo ya Mtanzania Anayecheza Nje Wanaume wanaowania ni Alphonce Mabulla (FC Shamakhi, Azerbaijan), Charles M'mombwa (Floriana FC, Malta), Haji Mnoga (Salford City, England), Mbwana Samatta (Le Havre, Ufaransa) na Novatus Miroshi (Göztepe FC, Uturuki).

Tuzo ya Mtanzania Anayecheza Nje Wanawake ni Clara Luvanga (Al-Nassr, Saudi Arabia), Diana Lucas (Trabzonspor, Uturuki), Hasnath Ubamba (FC Masar, Misri), Julitha Singano (Juárez FC, Mexico) na Opa Clement (SD Eibar, Hispania)