Prime
Fei Toto anavyoibua thamani ya wazawa
Muktasari:
- Fei Toto amebakiza msimu mmoja Azam, lakini mezani ana ofa nyingi kubwa ambazo akifanya uamuzi, kesho yake anaamka na jina jipya lenye hadhi ya kuitwa bilionea.
KAMA kuna mchezaji mzawa anayetarajiwa kumiliki mabilioni basi ni kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye wakati wowote thamani yake itaweka historia kuwa mchezaji ghali zaidi.
Fei Toto amebakiza msimu mmoja Azam, lakini mezani ana ofa nyingi kubwa ambazo akifanya uamuzi, kesho yake anaamka na jina jipya lenye hadhi ya kuitwa bilionea.
KIPI KINAMBEBA?
Fei Toto, ukiweka kando kipaji chake amejiweka ghali sokoni kutokana na mwendelezo wa kiwango. Sio rahisi kusikia au kuona kiungo huyo amecheza chini ya kiwango ambacho kimezoeleka.
Unaweza kuanzia wakati yupo Yanga alikuwa na kiwango bora akitumika mechi nyingi na hakuwa na rekodi ya kuandamwa na majeraha. Ukiwa na Fei Toto una uhakika kwamba atakuwa uwanjani katika mechi takribani zote. Hata alipohamia Azam FC, Fei Toto alitunza daraja lake la ubora, mara mbili mfulu-lizo akiibuka kinara wa ufungaji huku pia akinusa mfungaji bora wa ligi, akikosa kidogo tuzo ya MVP wa ligi.
Wachezaji wengi wazawa wamekuwa wakikwama kwa kukosa mwendelezo wa viwango. Hilo limeku-wa likiwanyima fursa ya kujitanulia thamani sokoni, kitu ambacho Fei Toto amekifanyia kazi na sasa anakitumia kuvuna fedha. Alitumika Yanga misimu mitano akifunga mabao 22, huku akiwakalisha ben-chi mastaa wa kigeni. Hata Azam alitikisa nyavu mara 19 msimu wa kwanza, wa pili nne na asisti 11 na wa tatu 15. Amefikisha jumla ya mabao 38 na asisti 11.
NIDHAMU JUU
Ukiacha kiwango chake, Fei Toto amebaki juu kwa ubora kutokana na nidhamu yake ndani ya uwanja na hata nje ya uwanja, imeshuhudiwa kwa miaka mitano amepata kadi moja nyekundu aliyoipata kati-ka mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Simba.Ukiondoa kadi hiyo, Fei Toto amekuwa na hati safi ya nidhamu ndani ya uwanja, lakini na nje ya uwanja hana mambo mengi anapo-kuwa kwenye maisha yake binafsi.
Akiwa nje ya uwanja imekuwa rahisi kumuona Fei Toto akiwa kwenye ratiba zake binafsi za mazoezi au kucheza soka la mtaani na watu wake, kitu ambacho ni tofauti na wazawa wengi ambao wamejikuta wakiangukia starehe tofauti zinazoharibu muendelezo wa vipaji vyao.
PESA INATANGULIA
Wapo wachezaji wazawa ambao waliingia kwenye mtego wa kupoteza thamani kutokana na mapenzi kwa klabu, lakini Fei imekuwa tofauti kitu anachotaka ni fedha ili aishi maisha mazuri baadaye.
Fei Toto aliondoka Yanga akilazimisha dili ili aende akapate fedha nyingi Azam FC iliyomuwekea dau kubwa mezani.
Akiwa Chamazi ameonyesha yupo tayari kurudi Yanga au Simba ikitegemea nani atamuwekea ofa kubwa mezani.
Inaelezwa kwamba kabla ya dirisha la usajili lililopita kufungwa, Fei Toto alikaribia kupata kiasi kisi-chopungua bilioni tatu kutoka kwa klabu za Simba na Yanga katika dau la kusaini mkataba na moja ya klabu hizo kongwe nchini na mshahara mkubwa.
Hapa maana halisi ambayo unaondoka nayo ni kwamba hana kingine anachokitaka katika kujiunga na timu yoyote zaidi ya fedha ambazo hata akistaafu zitamlinda kwa kujiendeleza maisha yake ya baadaye na kukimbia kuwa ombaomba.
AZAM IMEPANDA
Inaelezwa Azam imeshtuka na inataka kumpa mkataba mwingine zaidi, lakini dau ambalo wameliweka linaonekana wamejifunza kutoka kwenye ofa za Simba na Yanga, ikielezwa kwamba wanataka kumpa dau la Sh 5 bilioni.
UMRI WAKE
Fei Toto mpaka sasa amefikisha miaka 28, ambayo ukihesabu kwa makadirio unaweza kuona amebaki-sha miaka miwili mpaka mitatu kucheza soka la nguvu zaidi, ingawa kwa namna alivyo sasa anaweza kucheza hata zaidi ya hapo.
Miaka hiyo 28 ni wakati ambao anatakiwa kuanza kufikiria kama ikitokea anastaafu sasa atakuwa ame-andaa vipi maisha yake ya baadaye atakapoamua kustaafu? Hiki ndicho anachokifanya sasa, nina uhakika kwamba Fei Toto amebakiza muda mfupi kuwa bilionea kwa kusaini hapa ndani au hata nje ya nchi.
WASIKIE WADAU
Mchezaji wa zamani Simba, Dua Said, anasema kazi ya soka ni ya muda mfupi na mara nyingi hawapati muda wa kujiendeleza kielimu, kwa hiyo bila pesa ni ngumu kwao kuwa na maisha mazuri au kazi ya maana ya kujiendeleza.
“Wakati wetu tulikuwa tunacheza kwa kupenda timu ndio maana unaona kuna wachezaji wengi wa zamani ambao sasa hivi wamezeeka na umasikini kwa sababu hawakuwa na muda wa kufanya uwe-kezaji wa kutosha,” anasema Dua.
Mchezaji wa zamani Simba, Madaraka Seleman, anasema wachezaji wengi wamepata elimu kubwa kuhusu maisha baada ya kazi ya soka ambayo unaweza kustaafu kwa majeraha au miaka mingi uwan-jani.
“Mpira wa zamani haukuwa na pesa wala wadhamini kama ilivyo sasa, soka la wakati huu ni biashara ambayo inaweza kumtajirisha mchezaji kama atajielewa.”
Steven Mapunda aliwahi kuchezea Majimaji FC, Simba na Tiger FC, anasema: “Mpira ni biashara am-bayo inaweza kukulipa sana kama utaifanya vizuri.Wachezaji wa sasa wana nafasi ya kutajirika kupitia vipaji na nafasi wanazopata hasa kwenye hizi timu kubwa.”