Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI atakavyopitishwa kwenye presha Jangwani

Muktasari:

  • Yanga ilimuuza Aziz KI Wydad Athletic ya Morocco wakati ikielekea kumalizia msimu wa 2024/25, lakini hata hivyo hakufanikiwa kung’ara sana kwa Waarabu hao kisha baadaye kuuzwa tena kwa Al Ittihad ya Libya ambako nako alicheza kwa miezi sita na sasa Yanga imenunua tena ikimrudisha nyumbani.

STEPHANE Aziz KI ameanza maisha yake mapya baada ya kurejea klabu yake ya Yanga aliyoitumikia kwa mafanikio, baada ya kuwa nje ya klabu hiyo kwa msimu mmoja uliopita akizitumikia klabu mbili tofauti.


Yanga ilimuuza Aziz KI Wydad Athletic ya Morocco wakati ikielekea kumalizia msimu wa 2024/25, lakini hata hivyo hakufanikiwa kung’ara sana kwa Waarabu hao kisha baadaye kuuzwa tena kwa Al Ittihad ya Libya ambako nako alicheza kwa miezi sita na sasa Yanga imenunua tena ikimrudisha nyumbani.


Aziz KI amerejea Yanga na kurudishiwa jezi yake namba 10 aliyoivaa na kumpa mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo, mabosi wa klabu hiyo wakimuandaa kumtaka kuendelea kufanya makubwa, lakini haitakuwa rahisi sana kwani kuna mambo atatakiwa kupambana nayo kuthibitisha ubora wake.

REKODI YAKE YANGA
Aziz KI alifika Yanga mwaka 2022 na ndani ya misimu yake mitatu akawa mmoja wa wachezaji waliobe-ba timu hiyo katika eneo la ubunifu na ufungaji. Rekodi zake zinaonyesha alicheza mechi 114, akafunga mabao 52 na kutoa pasi 32 kabla ya kuondoka mwaka 2025. Pia alisaidia Yanga kushinda mataji tisa kati-ka kipindi chake cha kwanza klabuni hapo.


Msimu wa 2023/24 ndiyo uliomweka kwenye kilele cha soka la Tanzania. Aziz KI akifunga mabao 21 katika Ligi Kuu na kutwaa Kiatu. Lakini hakumaliza hapo, alitwaa pia tuzo ya MVP wa ligi pamoja na tuzo ya kiungo bora.


Hii ndiyo rekodi itakayomtesa kwa sasa, ambapo swali ambalo litakuwa kwenye vichwa vya mashabiki wa klabu hiyo ni kuona kama kiungo huyo fundi ataweza kurudia kufanya makubwa kama ambavyo alifanya kwenye msimu wake wa mwisho kabla ya kuondoka klabuni hapo.

WYDAD, AL ITTIHAD KARUDI NA NINI?
Baada ya kuondoka Yanga, Aziz KI alijiunga na Wydad 2025, akiwa huko mambo hayakwenda kwa ki-wango kile ambacho mashabiki wa Yanga walikuwa wamezoea. Takwimu za msimu wa 2025/26 zi-naonyesha alifunga bao moja, huku kwa upande wa mechi za kimataifa alicheza mechi mbili, baadaye alihamia Al Ittihad ya Libya, ambako alicheza kwa kipindi cha miezi sita.


Aziz KI hakuwa na muendelezo mkubwa akiwa kwenye klabu hizo mbili, kitu kikubwa ambacho anawe-za kujivunia ni kufanikiwa kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Klabu zilizofanyika nchini Marekani, lakini ubora wake na hata hadhi yake ilishuka kimtindo na sasa atarudi kujiuliza kuthibitisha daraja lake.

USHINDANI YANGA
Aziz KI ni jina kubwa anaporejea Yanga, ukaribisho wake wa juzi pale KMC Complex utathibitisha hilo, lakini haitakuwa rahisi kwake kupangua kikosi cha timu hiyo bila juhudi zake kubwa kwani timu hiyo imesheheni mafundi wa boli.


Kiungo huyo anatakiwa kutambua kwamba kuanzia alipoondoka, Yanga iliendelea kufanya vizuri na juzi tu pale Uwanja wa Amaani Zanzibar, klabu hiyo ilifunga kibabe Simba kwa bao 1-0 huku akiwa jukwaani.


Eneo la kiungo la Yanga lina watu bora ambao wanaweza kufanya makubwa, lakini bado Aziz KI ana da-raja lake la ufundi, anatakiwa kupambana kuhakikisha kipaji chake hicho kinambeba kwenye safari ya kurejea klabuni hapo.

MZIMU JEZI NAMBA 10
Jezi namba 10 yenyewe ni presha nyingine. Aziz KI amerudi Yanga na kupewa tena namba hiyo ambayo ina historia kubwa klabuni. Hii si namba ya kawaida kwa mashabiki wa Yanga. Ni namba inayobeba matarajio ya mchezaji anayetarajiwa kuwa chanzo cha ubunifu, pasi za mwisho na mabao.


Ndiyo maana kila mchezo utakuwa na kipimo chake. Akitoa asisti, itaonekana kama wajibu. Akifunga, itaonekana kama alichotakiwa kufanya. Akicheza vibaya, mjadala utakuwa mkubwa kwa sababu ata-hukumiwa dhidi ya Aziz KI aliyewahi kuonekana akiwa kileleni.

MOTO WA OKELLO BADO UNACHOMA
Kabla ya kurejea kwa Aziz KI, Yanga ilimwona Allan Okello akitoa mchango katika eneo la ubunifu. Takwimu zinaonyesha Okello alikuwa na mabao 14 katika mechi 18 za msimu wa 2025/26.


Hiyo ndiyo aina ya moto ambayo Aziz KI atakutana nayo. Mashabiki hawatasema tu, “Aziz KI amerudi.”  Watauliza, “Aziz KI anaweza kufanya zaidi ya tulichokiona kwa Okello?” 
Hapo ndipo presha inapopanda. Kwa sababu Aziz KI hatakiwi kurudi tu kuwa mchezaji mzuri. Anataki-wa kuwa mchezaji anayefanya Yanga iwe bora.

MBINU ZA KOCHA
Changamoto nyingine kwa Aziz KI ipo hapa, kwani anatakiwa kuhakikisha anaendana na falsafa za ko-cha mpya wa klabu hiyo, Manqoba Mngqithi.


Aziz KI si aina ya kiungo anayecheza kwa kukimbia bila mpira muda wote, nguvu yake kubwa iko kwenye akili ya kucheza wakati timu inamiliki mpira, kupokea, kugeuka, kutengeneza nafasi, kupiga pasi ya mwisho na kuingia eneo la hatari kwa wakati sahihi.


Kocha anataka timu iwe na presha kubwa, wachezaji wakimbie muda wote na kupambana katika kila eneo, Aziz KI atalazimika kubadilisha sehemu ya mchezo wake, hii haimaanishi hawezi kukimbia, ana-weza, lakini suala ni matumizi ya nguvu.


Mchezaji kama Aziz KI akitumia nguvu nyingi katika kukimbizana na wapinzani kila sekunde, anaweza kufika sehemu muhimu ya mwisho wa uwanja akiwa hana nguvu ya kufanya kitu chochote.

MAISHA YA NJE
Nje ya soka, Aziz KI ana sura tofauti, ikumbukwe raia huyu wa Burkina Faso ameoa hapa nchini, akiwa ni mume halali wa Mwanamitindo na Mwanamuziki Hamisa Mobeto, hapa kwa wakati huu makocha wa Yanga na mashabiki wa klabu hiyo wana kiu ya kuona kiungo huyo anaimbwa zaidi jina lake akiwa uwanjani kuliko maisha yake ya nje ya uwanja, kinyume na hapo atawavunja moyo wale ambao walikuwa na matarajio makubwa kwenye kurejea kwake nchini.


Aziz KI ana nafasi ya kuishinda presha hii endapo ataamua kuweka akili yake uwanjani na kubadilika ili kurudisha jina lake, kwani anarudi kwenye ligi ambayo anaijua, maisha ya Tanzania anayajua na kuya-kubali, mashabiki na viongozi wanamjua na kumkubali, sasa kazi iko kwake.