Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto aanza, KMKM waiwahi Yanga

Fei Toto aanza, KMKM waiwahi Yanga

Unguja. Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' leo ameanza kikosi cha kwanza kuikabili KMKM katika mchezo wao wa mwisho wa makundi ya Kombe la Mapinduzi.

Mechi hiyo inatarajia kuanza saa 10:00 jioni ya leo Alhamis ambapo mechi ya kwanza dhidi ya Taifa Jang'ombe ambayo ndiyo timu yake aliyotokea hakucheza kwani alipewa mapumziko.

Wakati Fei akianza kikosini tayari KMKM waingia Uwanjani saa 8:35 mchana kuwasubiri wapinzani wao Yanga walioingia 9.05 mechi itakayochezwa Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Kikosi cha Yanga hakina mabadiliko makubwa sana kwani kati ya walionzia benchi ni mmoja pekee Dickson Job ambaye leo ameanza akichukuwa nafasi ya David Bryson.

Kikosi cha Yanga kitakachoanza ni Aboutwalib Msheri, Paul Godfrey, Yassin Mustafa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Denis Nkane, Salum Abubakar, Heritier Makambo, Feisal Salum na Dickson Ambundo.

Upande wa KMKM ni Nassoro Abdalla Nassoro, Ahmed Is-haka Haji, Haji Mwinyi, Ibrahim Abdalla Hamad, Kheri Makame Jecha, Is-haka Said Mwinyi, Greyson Gwalala, Adam Abdalla, Abrahman Othman Ali, Optatus Yustin Lupekenya na Iliasa Suleiman Mohamed.